TANGAZO


Monday, November 18, 2013

Kinana atinga Songea na kukutana na waasisi wa TANU/CCM waliofanya mkutano wa siri na Baba wa Taifa Julius Nyerere 1957 wa kudai Uhuru wa Tanganyika


 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto) akiwavisha mgolole, Mzee Hashim Gawaza na Clement Nyoni alipotembelea Ofisi za CCM Kata ya Matogoro, Songea Mjini, wakati wa ziara ya kuimasha uhai wa chama na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya chama katika mikoa ya Ruvuma na Mbeya.  Wazee hao ni waasisi wa TANU na CCM na eneo hilo ndipo Baba wa Taifa, marehemu Julius Nyerere alifika na kufanya mkutano wa siri 1957 katika harakati zake za kupigania uhuru wa Tanganyika ambapo katika mkutano huo wazee hao walishiriki na wengine watano waliotangulia mbele ya haki.
 Katibu wa Siasa na Uhusiano wa Kimataifa wa NEC/CCM, Dk. Asha Rose Migiro 9katikati) akipiga picha ya kumbukumbu na wazee hao.
 Katibu wa NEC/CCM wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akiwa amekaa na baadhi ya wanachama wa shina namba moja linaloongozwa na Mjumbe Magreth Mtaula eneo la Mfaranyaki, mjini Songea leo. Kinana alitembelea shina hilo leo.

 Katibu wa NEC/CCM wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akiwa amekaa na baadhi ya wanachama wa shina namba moja linaloongozwa na Mjumbe Magreth Mtaula eneo la Mfaranyaki, mjini Songea leo. Kinana alitembelea shina hilo leo.
 Bibi Rose Haule akiwa na mwanawe huku akipeperusha bendera wakati wa mapokezi ya msafara wa Kinana eneo la Mletele Songea mjini leo.
 Kinana akisaidia kupiga lipu moja ya vyumba vya madarasa vinavyojengwa katika Shule ya Sekondari Mdandamo Songea Mjini leo.
 Baadhi ya wanachama wa CCM wakiungana na Kinana kuweka mazingira safi katika ujenzi wa Zahanati ya Mahilo, Songea mjini leo.
 Nape akizungumza na mmoja wa wanachama wa CCM, Felix Komba katika Kata ya Matogoro Songea Mjini leo.
 Wafuasi wa CCM wakiwa katika mkutano wa Shina namba moja ambapo Kinana alitembelea shina hilo na kuzungumza na wanachama.
 Mwasisi wa Tanu na CCM, Mustafa Songambele akisalimiana na Kinana alipokjutana naye katika Shina la CCM namba moja  eneo la Mfaranyaki, Songea Mjini Leo.
 Nape akisalimiana na Mzee Songamele
 Kinana akaimkabidhi mmoja wa vijana wapya wa CCM baada ya kuzindua tawi jipya la Dk. Asha Rose Migiro, eneo la Mfaranyaki, Songea mjini leo.
Kikundi cha Sanaa kikitumuiza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Tawi jipya la Vijana wa CCM la Dk. Asha Rose Migiro, eneo la Mfaranyaki, Songea Mjini leo. (Picha zote na Kamanda wa Richard Mwaikenda)

No comments:

Post a Comment