Kocha wa timu ya Taifa Kim Poulsen |
Na Boniface Wambura Mgoyo, Kaimu Katibu Mkuu
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
KOCHA
Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen ameunda kikosi cha wachezaji 32 kwa ajili ya
mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Kenya (Harambee Stars), itakayochezwa
Jumanne, Novemba 19 mwaka huu, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kikosi hicho, kinajumuisha wachezaji 16
walioitwa Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager, na wengine 16
kutoka Future Taifa Stars. Awali kambi ya Future Taifa Stars iliyoanza Novemba 9
mwaka huu na kuvunjwa leo asubuhi ilikuwa na wachezaji 30.
Wachezaji walioitwa ni
makipa wanne; Aishi Manula (Azam), Ally Mustafa (Yanga), Deogratias Munishi
(Yanga) na Ivo Mapunda (Gor Mahia, Kenya). Mabeki ni Aggrey Morris (Azam),
Ismail Gambo (Azam), Kelvin Yondani (Yanga), Michael Pius (Ruvu Shooting), Nadir
Haroub (Yanga) na Said Moradi (Azam).
Viungo wakabaji ni
Erasto Nyoni (Azam), Himid Mao (Azam), Shomari Kapombe (AC Cannes, Ufaransa) na
Vincent Barnabas anayechezea Mtibwa Sugar ya Morogoro.
Viungo ni Amri Kiemba
(Simba), Athuman Idd (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Haruna Chanongo, Hassan
Dilunga (Ruvu Shooting), Jonas Mkude (Simba), Ramadhan Singano (Simba), Salum
Abubakar (Azam) na William Lucian (Simba).
Viungo washambuliaji ni
Faridi Musa (Azam), Joseph Kimwaga (Azam), Mrisho Ngasa (Yanga), Mwinyi Kazimoto
(Markhiya, Qatar) na Simon Msuva (Yanga).
Washambuliaji ni Elias
Maguli (Ruvu Shooting), Juma Liuzio (Mtibwa Sugar), Mbwana Samata (TP Mazembe, DRC)
na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC).
No comments:
Post a Comment