Mchungaji Abrahim Kiyinga toka Kanisa la Christ Embassy (kushoto) akisistiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) leo, jijini Dar es Salaam, juu ya huduma za afya zitakazotolewa na kanisa hilo siku kesho katika viwanja vya Biafra, katikati ni Kiongozi Mkuu wa Kanisa la Christ Embassy Mchungaji Ken Igini na mwisho ni Mchungaji Fredy Rwegasira.
Baaadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini Kiongozi Mkuu wa Kanisa la Christ Embassy Mchungaji Ken Igini (hayupo pichani) wakati akielezea juu ya huduma ya afya itakayotolewa na kanisa hilo kesho katika Viwanja vya Biafra. (Picha zote na Eliphace Marwa - MAELEZO)
Na Eliphace Marwa - Maelezo
Kanisa la Christ Embassy linatarajia kuendesha zoezi la
kutoa huduma za afya kwa wakazi wa Dar es Salaam siku ya kesho katika viwanja
vya Biafra, kinondoni jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari mapema hii leo jijini Dar
es Salaam Mkuu wa Kanisa hilo Tanzania Mchungaji Ken Igini amesema kuwa lengo
la kutoa huduma hiyo ya afya kwa wakazi wa Dar es Salaam ni sehemu ya
kusherehekea siku ya kuzaliwa kwa kiongozi mkuu wa kanisa hilo duniani
Mchungaji Chriss Oyakhilome.
“Kanisa la Christ Embassy limeamua kutoa huduma ya afya kwa
wananchi ikiwa ni sehemu ya kusherehekea kuzaliwa kwa kiongozi wetu mkuu Mchungaji
Chriss Oyakhilome”, alisema Mchungaji Ken Igini.
Aidha Mchungaji Ken aliongeza kuwa ni imani yao kuwa watu
watajitokeza kwa wingi kwani matarajio yao ni kuhudumia zaidi ya watu elfu
moja kwani kutakuwa na madaktari wa
kutosha kwa ajili ya kutoa huduma hiyo.
“Tunatarajia kupata wataalam kutoka sehemu mbalimbali ikiwemo
wizara ya afya na taasisi zingine ambazo zimeonesha nia ya kushirikiana na
kanisa la Christ Embassy katika kutoa huduma hii kwa watanzania wenye mahitaji”,
alisema Mchungaji Ken Igini.
Naye Mchungaji Abrahim Kiyinga alisema kuwa endapo watu
watajitokeza kwa wingi wataongeza siku ya kutoa huduma ya afya kwa watu wenye
shida ya kupata huduma hiyo.
“Ni matarajio yetu kuwa watu watakuja kupima kwa wingi sana
kwani huduma hizi ni bure kabisa na tutaanza kutoa huduma za vipimo vya
magonjwa mbalimbali kuanzia saa tatu asubuhi”, alisema Mchungaji Abrahim
Kiyinga.
Sherehe hii ya kuazaliwa kwa Kiongozi mkuu wa kanisa la
Christ Embassy zinasherehekewa na makanisa yote ya Christ Embassy Dunianiani
kwa kufanya shughuli mbalimbali ikiwa ni sehemu ya kusherehekea siku hiyo.
No comments:
Post a Comment