Umoja wa Mataifa unajiandaa kuanza utafiti kwenye kambi kubwa
ya wakimbizi duniani ya Dadaab iliyopo Kaskazini mwa Kenya ili kujua wakimbizi
karibu nusu milioni kutoka Somalia waliopo kwenye kambi hiyo ambao wapo tayari
kurejea nchini mwao.
Mwandishi wa Habari wa BBC aliyepo kwenye kambi hiyo anasema ni wakimbizi wachache chini ya mia moja ambao wapo tayari kurejea nchini mwao, ambapo wengi wanasema hali ya usalama nchini Somalia bado ni hatari kutokana na kuwepo kwa wapiganaji wa Kiislamu.
Kuwepo kwa wakimbizi imezusha wasiwasi wa kisiasa nchini Kenya kufuatia shambulio la Septemba ambapo wapiganaji wanaodaiwa kuwa ni wa Kisomali kushambalia kituo cha biashara cha Westgate ambapo watu 67 waliuawa.
Serikali ya Kenya imesema miaongoni wa walioendesha shambulio hilo ni wakimbizi kutoka kwenye kambi hiyo ya Daadab.
No comments:
Post a Comment