TANGAZO


Monday, November 11, 2013

Gharika yasababisha maafa Puntland

Rais wa eneo la Somalia lililojitenga la Puntland ameiambia BBC kuwa takriban watu mia moja wamekufa kutokana na gharika mwishoni mwa juma.
Abdirahman Farole amesema kuwa maelfu ya mifugo wamekufa na mamia ya makao ya watu kuharibiwa.
 
Amesema kuwa juhudi za kupeleka chakula katika maeno yaliyoathiriwa zinaendelea.
Eneo hilo lilikumbwa na upepo mkali,mvua kubwa na mafuriko na mji wa bahari wa Ely ndio uliathirika zaidi. Baadhi ya wavuvi hawajulikani waliko.
Hali hiyo pia ilikumba maeneo ya Gardafu na Bender Beyla. Gavana wa Gardafu Ali Mire anasema mtu mmoja amekufa na mashamba kuharibiwa. Biashara ya uvuvi pia imeathiriwa vibaya.

Maeneo kadhaa yakiwemo Gardafu, Bender Beyla na Eyl na maeneo mengine yaliyo Kaskazini Mashariki ya Nugaal na Bari yalishuhudia mvua kubwa na upepo mkali.

Gavana wa jimbo la Gardafu District Ali Mire, aliongeza kuwa mvua kubwa imeathiri pakubwa shughuli za uvuvi huku baadhi ya wakaazi wakiwa hawajulikani waliko.

Gharika ilitarajiwa kuathiri pakubwa maeneo ya Eyl na Nugaal ambako kumekuwa na uhaba wa mvua.
Pia maeneo yaliyoathirika na mvua hiyo yangali kupata msaada kutoka nje.

No comments:

Post a Comment