Aliyekuwa Rais wa Liberia Charles Taylor, ameomba ahudumie kifungo chake cha miaka hamsini kwa makos aya uhalifu wa kivita nchini Rwanda wala sio Uingereza kama ilivyokuwa imsemekana hapo awali.
Katika barua yake kwa mahakama iliyomuhukumu, anasema kuwa itakuwa rahisi kwake na familia yake kwani haitawagharimu sana ikiwa watakuwa wanakuja kumtembelea gerezani Afrika kuliko Uingereza.
Pia alielezea hofu ya kushambuliwa ndani ya gereza la Uingereza.
Taylor alihukumiwa miaka hamsini jela kwa kuwasaidia waasi wa Sierra Leone kifedha katika kufanya maasi nchini mwao wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe Sierra Leone.
Wiki jana waziri wa mambo ya ndani nchini Uingereza alithibitisha kuwa Taylor atatumikia kifungo chake gerezani nchini Uingereza.
Mahakama ya Umoja wa Mataifa kuhusu kesi za Sierra Leone ilimpata na hatia Taylor , lakini kesi yake ilifanyika katika mahakama mjini Hague kwa hofu ya kuzua vurugu zengine Magharibi mwa Afrika.
Uholonzi ilikubali tu kuendesha kesi hiyo sharti afungwe katika nchi nyingine yoyote ile.
No comments:
Post a Comment