Maafisa nchini Uganda wamekamata shehena meno ya tembo yenye
uzito wa tani mbili, ambacho ni kiwango kikubwa kukamatwa kwa miaka mingi
iliyopita.
Kuna mahitaji ya meno ya tembo kutoka barani Afrika kwenda nchi Asisa kwa ajali ya kutengeneza mapambo.
Meno hayo ya tembo yalikuwa yakielekea kwenda katika bandari ya Mombasa nchini Kenya.
Baadhi ya meno hayo yalikuwa yamekatwa vipande vipande na kufunikwa chupa za plastiki kwenye kreti na kubandikwa maandishi kwamba na bidhaa zinazokwenda kuchakatwa.
Chama hicho cha Wanyama pori kimemwambia mwandishi wa habari wa BBC Catherine Byaruhanga kuwa Uganda imeanza kutumika na majangili kama njia ya kupitisha bidhaa za wanyapori kutoka nchi za Sudan Kusini na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
No comments:
Post a Comment