TANGAZO


Saturday, October 5, 2013

Mkutano kujadili maafa ya Lampedusa


Mkimbizi akinusuriwa nje ya Lampedusa
Ufaransa imeitisha mkutano wa haraka wa nchi za Umoja wa Ulaya baada ya mashua kuzama nje ya Utaliana ambapo inafikiriwa wakimbizi zaidi ya 300 kutoka Afrika wamekufa .
Waziri Mkuu wa Ufaransa, Jean-Marc Ayrault, alisema huruma haitoshi - wanasiasa wa Ulaya lazima watafute suluhu inayofaa.
Huku nyuma meya wa Rome, Ignazio Marino, amejitolea kuwaweka mjini humo manusura 150 wa maafa hayo.
Miili zaidi ya 100 imeopolewa kutoka baharini lakini mawimbi yanazuwia msako wa abiria wengine 200 ambao wametoweka.

No comments:

Post a Comment