siku chache kutimiza mwaka tangu wazaliwe. (Picha zote na John Banda)
Rehema Khamis akiwa na watoto wake mapacha watatu na dada yao ambapo hata hivyo kaka yao hakuwe mwenye
umri wa miaka 13, mama huyo anahitaji msaada ili aweze kuwatunza kuwalea.
Rehema Khamis(30) akimlisha uji mtoto mmoja kati ya mapacha watatu huku wengine wakisubirishwa mpaka wa kwanza amalize kulishwa na mama huyo kukosa mtu wa kumsaidi kuwalea watoto hao.
Rehema Khamis (30)akimlisha uji mtoto mmoja kati ya mapacha watatu huku wengine wakisubirishwa mpaka wa kwanza amalize kulishwa na mama huyo kukosa mtu wa kumsaidi kuwalea watoto hao.
Na John Banda,
Dodoma
MWANAMKE wa
mwanajeshi anaomba msaada kwa wasamaria wema ili aweze kuwahudumia watoto wake watatu aliojifungua kwa
chakula, mavazi na elimu kutokana na ugumu wa maisha unaomkabili pamoja na familia yake, kiasi cha kushindwa kupata
hata lishe ya kuwapa mapacha hao watatu, kinyume na matarajio yake.
Mwanamke huyo,
Rehema Khamis (30), mkazi wa Mkalama, Kata ya Makulu, Manispaa ya Dodoma, ameomba
msaada huo baada ya kuona tokea alipojifungua watoto hao, watatu imefika wakati hata
kushindwa kuwapatia hata uji wenye lishe huku mshahara wa mumewe huyo ukiishia
kwenye madeni anayodaiwa na watu.
Rehema alisema
kuwa tokea alijifungua watoto hao, wa kiume wawili na wa kike mmoja, ambao ni Hassan,
Hussein na Hasanati katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma, ambapo sasa wanakaribia kuwa
na umri wa mwaka mmoja, amekuwa akikabiliana na matatizo mengi hadi kulazimika kuwaachisha kunyonya wakiwa na miezi 7 kutokana na
kukosekana maziwa ya kutosha.
Alisema
kuwa hakutarajia kupata watoto watatu kwa mpigo kutokana na kuwa tayari alishakuwa na
wengine wawili, hivyo alijua akipata mmoja angepumzika kuzaa ili ajipe nafasi ya
kuwalea, hivyo kutokana na watoto hao kuhitaji chakula, mavazi na hata elimu wawapo wakubwa.
‘’Watu wa
kada mbalimbali wamekuwa wakifika kuwaona watoto wangu hawa lakini ni kama uwanja wa
maonyesho tu kwani hakuna hata mtu mmoja aliyekuja kutuona na kasha kutusaidia chochote, watu wanafika kutuona na kisha kuondoka bila
kuleta msaada wowote, hivyo ninawaomba wenye uwezo na moyo waweze kutusaidia chochote ili watoto hawa waweze
kupata malezi bora", alisema Rehema.
Nae Baba wa
watoto hao Abubakari Ally Hamad Mwanajeshi wa ajira mpya katika jeshi la
wananchi wa Tanzania [JWTZ] kikosi cha 673 Msalato Dodoma alisema mahitaji
yamekuwa hayatoshelezi kutokana na mshara anaopata kuishia kwenye madeni ambayo
amekuwa akikopa kwa wanajeshi wenzake.
Alisema pesa
hata madeni hayo ambayo amekuwa akikopa hayatoshelezi mahitaji ya watoto hao
ambao hata hivyo hahitaji kuongeza wengine, hata hivyo aliwataka watu mbalimbali
zikiwemo taasisi za kiserikali kumsaidia kutokana na watakavyojaliwa na mwenyezi
mungu ili aweze kuwa tunza watoto wake.
Kwa upande
wake Ofisa mtendaji wa kijiji cha makulu Namsfu Mihungo alisema wao kama
serekali wanajitahidi kufikisha ujumbe kwa watu kuhusu familia hiyo kuhitaji
msaada na kufika kuwaona lakini hawakujua kama hakuna msaada unaotolewa, hivyo
watajipanga kuona nini watafanya ili kuisadia familia hiyo kwa kadili
watakavyoweza.
No comments:
Post a Comment