Naibu Msajili Mwandamizi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, John Kahyoza akielezea mikakati ya Mahakama hiyo, kutumia mfumo wa TEHAMA, ili kuongeza kasi ya uendeshaji wa mashauri. Katikati ni Ofisa Habari wa Mahakama ya Tanzania, Mary Gwera na kulia ni Ofisa Habari wa Idara ya Habari (Maelezo), Frank Mvungi. (Picha zote na Eliphace Marwa - MAELEZO)
MAHAKAMA ya Tanzania ni moja kati ya Mihimili
mitatu ya Dola, na majukumu yake makubwa kwa mujibu wa Katiba ni Kutafsiri
sheria na kutolea maamuzi kesi mbalimbali zinazoletwa Mahakamani.
107A:- (1) Sura ya tano ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
inasomeka kuwa:
‘Mamlaka yenye kauli ya mwisho ya utoaji haki
katika Jamhuri ya Muungano itakuwa ni Mahakama.’
Kufuatia jukumu hili muhimu Mahakama imejiwekea dira ambayo ni; ‘Kutoa
haki sawa kwa wote na kwa wakati.’
Hata hivyo; Mahakama ya Tanzania imekuwa
ikikabiliwa na changamoto kadhaa likiwemo suala zima la uendeshaji wa shughuli zake
za kila siku.
Hata hivyo Mahakama ya Tanzania,imefanikiwa kwa kiasi kikubwa, kufuatia
hatua na michakato mbalimbali ambayo tayari imekwishafanyika na mingine ikiwa
kwenye hatua nzuri yote yakiwa yanalenga katika kuboresha huduma ya utoaji haki
nchini.
MAFANIKIO YALIYOFIKIWA NA MAHAKAMA YA TANZANIA.
i.Kurejewa
kwa Muundo wa Mahakama na kuandaa Muundo
mpya wa
Utawala wa Mahakama uliopitishwa katika Sheria mpya ya Uendeshaji wa Mahakama (The Judicial Administration Act, No.4/2011).
Kwa mujibu wa muundo huu Shughuli za Kiutawala na za
Kimahakama zimetenganishwa, Mhe. Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania
atasimamia shughuli za Mahakama tu, wakati Mtendaji Mkuu (Chief Court
Administrator) atashughulikia masuala ya Kiutawala. Muundo huu mpya tayari umeanza kutekelezwa
rasmi katika mwaka wa fedha uliopita, 2012/2013. Hatua hii itaboresha na
kuongeza ufanisi katika shughuli za utoaji haki nchini.
Mchakato
wa mabadiliko ya Muundo wa Mahakama ulianza miaka 16 iliyopita kufuatia ripoti
ya Kikosi kazi kilichoongozwa na Mhe. Jaji Mark Bomani ambayo ilipendekeza
kufanyika kwa mabadiliko ya Muundo wa Mahakama ili kuboresha ufanisi katika
utendaji kazi wa Mhimili huu muhimu.
ii.Uanzishwaji wa Mfuko wa Mahakama chini ya Sheria ya
Uendeshaji
wa Mahakama Na.4 ya mwaka 2011. Lengo la mfuko huu ni kuwezesha uendeshaji wa
mashauri katika Mahakama za ngazi zote kwa kuboresha mfumo wa usikilizaji wa
Mashauri katika Mahakama za ngazi zote kwa kuboresha mfumo wa usikilizaji
Mashauri na ununuzi wa vitendea kazi.
Kuanzishwa
kwa Mfuko wa Mahakama kumesaidia kuongezeka kwa bajeti ya Mahakama kutoka
bilioni 20 kwa bajeti ya mwaka wa fedha 2011/12 kuwa bilioni 30 kwa bajeti ya
2012/13 na kuwa bilioni 140 kwa bajeti ya mwaka 2013/14.
Aidha,
Mfuko umesaidia kuharakisha kasi ya usikilizaji wa mashauri na idadi ya vikao
vya Mahakama. Vikao vya Mahakama ya Rufani vimeongezeka kutoka 22 kwa mwaka wa
fedha 2012/13 hadi 30 kwa mwaka huu wa fedha. Huku rufaa zilizomalizika
zikiongezeka kutoka 585 hadi 634 hadi kufikia mwezi wa Septemba 2013. Mahakama
ya Rufani inakusudia kumaliza rufaa 1200 kwa mwaka 2014. Mahakama Kuu yenye
kanda 13 na inatarajia kumaliza mashuri 11000 wakati kwa mwaka jana illimaliza
mashauri 5600 na kutolea maamuzi mashauri. Mahakama Kuu hadi kufikia mwezi Juni
mwaka huu mahakama tayari ilikuwa imepokea mashauri mapya 1402 na kumaliza mashauri
1781 kati ya hayo 936 akiwa ya jinai na 489. yakiwa ya madai na yaliyobakia
yakiwa ni mashauri ya jinai yaliko katika masjala za kawaida.
Utaratibu
huu pia umesaidia kuharakisha upatikanaji wa nakala za mwenendo wa Mashauri na
hukumu pamoja na kuwarahisishia kazi Majaji na mahakimu wanaosikiliza kesi
katika Mahakama hii. Mfuko huu pia utasaidia katika kuboresha miundombinu ya
Mahakama hususani Majengo, Vitendea kazi, maslahi ya Watumishi n.k.
Mfuko
umewezesha kufufuliwa kwa vikao vya kusukuma kesi na mashauri. Vikao hivi ni
muhimu kwani hukusanya wadau na kujadili mbinu za kupunguza mashauri yenye muda
mrefu mahakamani. Bajeti ya kuendesha vikao hivyo kwa ngazi mbali mbali za
mahakama imetengwa na tayari vikao hivyo vimeanza kufanyika.
iii.Upatikanaji wa fedha za O.C kadri ya Bajeti ilivyopangwa.
iv.Uanzishwaji wa zoezi la nchi nzima la utunzaji bora wa kumbukumbu, ukusanyaji wa Takwimu na matumizi yake na kuingiza mpango kamili wa matumizi ya TEHAMA kwenye shughuli.
v.Kufanyika kwa vikao vya Mahakama ya Rufani na Mahakama Kuu (Court sessions kwa asilimia 100).
vi.Kuanzisha programu maalum ya uondoshaji wa mashauri ya muda mrefu Mahakamani.
vii.Kukamilishwa kwa ujenzi wa jengo la Mahakama Kuu Bukoba na kuzinduliwa rasmi na Mhe. Rais Jakaya M. Kikwete mnamo tarehe. 25, Julai, 2013.
viii.Uboreshwaji wa posho za Wazee wa Baraza kutoka 1,500 hadi kufikia Shilingi 5000 kwa kila shauri linalohitimishwa.
ix.Kuajiri jumla ya Mahakimu 300 wahitimu wa Shahada ya kwanza ya Sheria na kuwasambaza kwenye vituo vya Mahakama za Mwanzo katika wilaya 102. Hatua hii imesaidia tatizo lililokuwepo la upungufu wa Mahakimu wa Mahakama za Mwanzo.
x.Miradi ya ujenzi.
Aidha, Mahakama ya Tanzania inaendelea na mchakato wa kuanza kwa ujenzi
wa majengo ya Mahakama katika ngazi mbalimbali.
·Ujenzi wa
Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania.·Ujenzi wa Mahakama Kuu katika Mikoa tisa; ambayo ni Mtwara, Kigoma, Mara, Lindi, Morogoro, Manyara, Singida, Shinyanga na Dodoma.
·Kuanza kwa ujenzi wa Mahakama ya Wilaya ya Bunda, Bariadi, Nkasi, Bukombe, Bagamoyo na Kilindi.
·Kuanza kwa ujenzi wa Mahakama ya Mwanzo Buguruni, Kawe, Kigamboni, Makuyuni, Maili Moja, Songea, Mpanda, Terrati, Mtowisa, Sangabuye, Ilolankulu, Mwanga, Mangaka, Makongolosi, Itigi, Machame, Mkomazi, Gairo, Kiagata, Lukuledi na Longido; pamoja na ujenzi wa Mahakama za Mwanzo Ngorongoro, Kolekero, Magoma na Bomang’ombe.
MIKAKATI YA MAHAKAMA
·Dhamira ya
Mahakama ni kuondoa mashauri/kesi zote zenye umri zaidi ya miaka miwili (2).·Kuboresha takwimu za mashauri/ kesi zilizopo Mahakamani.
·Kuboresha na kusimamia masjala.
·Kudhibiti kalenda za vikao ‘Court Sessions’.
·Kuweka “Benchmarks” kwa maofisa wa Mahakama katika kumaliza mashauri kwa wakati.
·Kuboresha kanuni za kuendesha mashauri.
·Kuimarisha utawala na usimamizi wa mashauri.
Pamoja na Mafanikio tajwa; jitihada za dhati bado zinaendelea kufanyika
katika kuhakikisha kuwa Mahakama inajengewa mazingira bora ya kufanyika kazi, kufanikisha
jukumu la Utoaji Haki kwa wakati nchini.
Asanteni kwa kunisikiliza.
Contact; Mary Gwera. (0756 866533/marygwerac@yahoo.com)Afisa Habari
Mahakama ya Tanzania
No comments:
Post a Comment