Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mkewe, Mama Salma, Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) jana, wakati alipowasili katika viwanja vya mahafali katika mahafali ya Kwanza ya Shule ya Sekondari ya WAMA Nakayama, yaliyofanyika shuleni katika Kijiji cha Nyamisati, Wilaya ya Rufiji, mkoani Pwani jana. Zaidi ya wanafunzi 60 walitunukiwa vyeti vya kumaliza kidato cha nne na zawadi mbalimbali zilitolewa kwa wahitimu wakati wa mahafali hiyo, ambayo yalihudhuriwa pia na viongozi na watu mashuhuri, akiwemo Balozi wa Japan na wafanyabiashara, ambapo Mwenyekiti wa IPP, Reginald Mengi aliahidi kuisadia shule hiyo, shilingi milioni 200 kila mwaka kwa miaka mitano mbazo ni kiasi cha shilingi bilioni moja kwa miaka hiyo mitano. (Picha zote kwa hisani ya Fullshangwe)
Rais Jakaya Kikwete akizungumza na wageni waaikwa na wahitimu wakati wa mahafali hayo jana huko Nyamisati Rufiji.
Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mkuu wa shule ya WAMA Nakayama Suma Mensa na viongozi mbalimbali wakati aliowasili shuleni hapo.
Watu mashuhuri na viongozi mbalimbali wakiwa katika mahafali hayo.
Mama Salma Kikwete akiwasili katika eneo la tukio. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya Shule hiyo Dk. Ramadhan Dau.
Wahitimu wakiingia katika eneo la tukio.
Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete akicheza na wanawake wenzake wake wa viongozi.
Rais Jakaya Kikwete wa nne kutoka kulia akiwa na viongozi mbalimbali katika meza kuu wakiimba wimbo wa taifa uliooongozwa na wanafunzi wa shule ya WAMA Nakayama kutoka kulia ni Balozi anzania Mhe.Masaki Okada Mkuu wa mkoa wa Pwani Ndugu Mwantumu Mahiza, Mama Salma Kikwetena kutoka kushoto ni Dr. Ramadhan Dau Mwenyekiti wa bodi ya shule ya Wama Nakayama na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dr. Shukuru Kawambwa.
Baadhi ya wanakamati kutoka kulia ni Teddy Mapunda Mkurugenzi wa Kampuni ya Montage, Daudi Nasibu Katibu Mkuu wa Taaisis ya WAMA na Dan Kiondo.
Baadhi ya wananfunzi wa shule ya WAMA Nakayama.
Mbunge Vick Kamata akiongoza wanafunzi wa Wama Nakayama kuimba wimbo maalum kwa wahitimu katika mahafali hayo.
Viongozi mbalimbali wakicheza muziki wakati wa mahafali hayo.
Dk. Ramadhan Dau, Mwenyekiti wa bodi ya shule ya Wama Nakayama akizungumza katika mahafali hayo
Mama Salma Kikwete akikaribisha wageni mbalimbali katika mahafali hayo.
Mkuu wa shule ya WAMA Nakayama Suma Mensa aakitoa historia ya shule hiyo
Mmoja wa wasanii wa kundi la Mjomba Band linaloongozwa na msanii Mrisho Mpoto akiigaiiza katika igizo maalum lililokuwa likitafsiri changamoto zinazomkabili mtoto wa kike yatima na anayeishi kwenye mazingira magumu katika suala zima la kupata elimu.
Mkuu wa Wilaya ya Kionondoni, Jordan Rugimbana pamoja na waalikwa wengine (katikati), akiwa katika hafla hiyo.
Wahitimu wakiimba wimbo maalum wa kumshukuru Mwenyekiti wa WAMA mama Salma Kikwete.
Nyoka alikuwa ni moja ya burudani katika mahafali hayo.
Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Regnald Mengi akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza. Kulia ni mke wa Makamu wa Rais, Mama Aisha Bilal.
Baadhi ya majengo ya shule hiyo.
Rais Jakaya Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete akicheza wimbo maalum ulioimbwa na wanafuzni wahitimu katika mahafali hayo
Rais Jakaya Kikwete na Mkewe mama Salma Kikwete wakiongoza viongozi mbalimbali kucheza wimbo huo
No comments:
Post a Comment