Rais wa Kenya anasema nchi yake huenda ikabidi 'kuingilia kati nje' ili kuilinda Kenya na majirani zake.
Rais Uhuru Kenyatta amesema hayo karibu mwezi baada ya shambulio katika jumba la maduka la Westgate mjini Nairobi ambapo watu kama 67 waliuwawa.
Kenya tayari ina wanajeshi wanaopigana na Al Shabab nchini Somalia.Wapiganaji Waislamu wa Somalia, Al Shabab, wamedai kufanya shambulio hilo.
Rais Kenyatta alisema Kenya iko tayari kuchukua hatua wakati wowote inapohitajika, ingawa hakutoa maelezo zaidi.
Alisema Wakenya wataimarisha usalama nyumbani, kwa kuwa waangalifu.
No comments:
Post a Comment