TANGAZO


Monday, October 14, 2013

Haramia sugu akamatwa Ubelgiji



Baadhi ya maharamia wa kisomali waliokamatwa na kufungwa jela katika nchi za kigeni
Mtu anayesemekana kujigamba kuwa haramia wa kisomali na anayejulikana kwa jina Afweyne au (Big Mouth) amekamatwa nchini Ubelgiji.
Big Mouth, ambaye jina lake halisi ni Mohamed Abdi Hassan, alitangaza mwezi Januari kuwa alikuwa anaasi uharamia baada ya miaka mingi katika biashara hiyo haramu.
Anasemekana kupata mamilioni ya dola kwa kazi yake ya kuongoza maharamia wenzake kuteka nyara meli.
Vyombo vya habari nchini Ubelgiji vinasema kuwa Big Mouth anashukiwa kuhusika na utekaji nyara wa meli kubwa ya Ubelgiji kwa jina 'Pompei' mnamo mwaka 2009.
Uharamia nchini Somalia umepungua katika miaka ya hivi karibuni baada kudhibitiwa kwa dori katika fuo za bahari.

No comments:

Post a Comment