TANGAZO


Thursday, August 8, 2013

Waingereza washambuliwa Zanzibar


Ni mara ya kwanza kwa shambulizi kama hili kutokea Zanzibar
Polisi katika kisiwa cha Zanzibar wamesema wanawake wawili wa Uingereza wamerushiwa maji ya Acid katika nyuso zao baada ya kuvamiwa mwendo wa usiku.
Naibu kamishna wa polisi amesema kuwa wanaume wawili waliwatendea wanawake hao Katie Gee na Kirstie Trup, wote wenye umri wa miaka 18 kutoka London,kitendo hicho walipokuwa wakitembea katika barabara za mji wa kihistoria wa zanzibar.
Wanawake hao ni walimu wa kujitolea wakifanya kazi kisiwani humo
Amesema kuwa polisi tayari wameanzisha msako dhidi ya wanaume hao.
Katika taarifa yake shirika la usafiri la i-to-i nchini Uingereza lilisema kuwa wanawake hao wameondoka hospitalini.
Kwa upande wake wizara ya mambo ya ndani Uingereza ililezea wasiwasi kuhusu mashambulizi dhidi ya raia wake na kuwa tayari imetoa msaada kwao kupitia kwa ubalozi wake.
Wanawake hao, wanasemekana kufanyia kazi shirika moja la kujitolea na nia ya shambulizi hilo haijulikani.
Polisi wanasema kuwa wanawake hao wenye umri wa miaka 18 walikuwa wakitembea katika mji wa Mawe kisiwani Zanzibar ambao ni kivutio kikuu cha utalii kisiwani humo, wakati wanaume wawili waliokuwa wamepanda piki piki walipowamwagia Acid kwenye mikono , vifua na nyuso zao.
Wanawake hao walipelekwa kwa ndege hadi Dar es Salaam ambako walipokea matibabu . Afisa wa wizara ya afya amesema kuwa majeraha yao si ya kutishia maisha .
Polisi wa Zanzibar wamesema ni mara ya kwanza kwa raia wa kigeni kushambuliwa kwa namna hiyo na kwamba wanawasaka wahusika.
Zanzibar ni kisiwa kinachokaliwa na idadi kubwa ya waislam na shambulio hilo linakuja katika kipindi cha mwisho wa mwezi mtukufu wa Ramadhan , wakati watu wakisherehekea sherehe za Eid

No comments:

Post a Comment