
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Inspekta Jenerali, Said Mwema (kushoto) pamoja na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Uturuki, Zeki Catalakaya (katikati) wakisaini hati ya ushirikiano wa kuchunguza matukio ya uhalifu kati ya Tanzania na Uturuki. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi akilishuhudia tukio hilolililofanyika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, jijini Dar es Salaam jana.

Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Uturuki, Zeki Catalakaya (kulia) akimkabidhi ufunguo wa gari la kuchunguza matukio ya uhalifu, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi. Tukio hilo la makabidhiano lilifanyika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, jijini Dar es Salaam jana.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi akiliwasha gari maalumu la kuchunguza matukio ya uhalifu mara baada ya kukabidhiwa ufunguo na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Uturuki, Zeki Catalakaya. Gari hilo ambalo linavifaa vyote vya kuchunguza matukio ya uhalifu nchini lilikabidhiwa jana Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, jijini Dar es Salaam

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi akiwashukuru kwa furaha ujumbe kutoka nchini Uturuki baada ya kukabidhi gari maalumu ya kuchunguza matukio ya uhalifu nchini kwa Jeshi la Polisi. Gari hilo ambalo linavifaa vyote vya kuchunguza matukio ya uhalifu nchini lilikabidhiwa jana Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, jijini Dar es Salaam

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi akizungumza na ujumbe kutoka nchini Uturuki pamoja na maofisa wa Jeshi la Polisi wakati wa hafla fupi ya kusaini hati ya ushirikiano wa kuchunguza matukio ya uhalifu kati ya Jeshi la Polisi nchini na Jeshi la Polisi la nchini Uturuki. Tukio hilo limefanyika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, jijini Dar es Salaam jana.

No comments:
Post a Comment