Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua rasmi Kongamano la Jumuiya ya Afrika Mashariki katika kuadhimisha Siku ya Mabunge Duniani, kuhusu suala la Makazi. Kongamano hilo limefunguliwa leo Agosti 19, 2013 jijini Arusha.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipanda mti wa kumbukumbu katika eneo la Ukumbi wa Bunge la Afrika Mashariki, baada ya kufungua rasmi Kongamano la Jumuiya ya Afrika Mashariki katika kuadhimisha Siku ya Mabunge Duniani, kuhusu suala la Makazi, lililofunguliwa leo Agosti 19, 2013 jijini Arusha.
Baadhi ya wabunge na wageni waliohudhuria ufunguzi wa Kongamano hilo leo, jijini Arusha.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuzindua Maonyesho ya Kongamano la Jumuiya ya Afrika Mashariki katika kuadhimisha Siku ya Mabunge Duniani, kuhusu suala la Makazi. Kongamano hilo limefunguliwa leo Agosti 19, 2013 jijini Arusha. Kulia ni Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makzi, Prof. Anna Tibaijuka.
Baadhi ya wabunge na wageni waliohudhuria ufunguzi wa Kongamano hilo leo, jijini Arusha.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuzindua Maonyesho ya Kongamano la Jumuiya ya Afrika Mashariki katika kuadhimisha Siku ya Mabunge Duniani, kuhusu suala la Makazi. Kongamano hilo limefunguliwa leo Agosti 19, 2013 jijini Arusha. Kulia ni Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka.
Baadhi ya wabunge na wageni waliohudhuria ufunguzi wa Kongamano hilo leo, jijini Arusha.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja Masoko wa Kampuni ya Tree Ltd ya Arusha, Magdalena Ayo, kuhusu utengenezaji wa Majiko Bomba, wakati Makamu alipokuwa akitembelea katika mabanda ya maonyesho ya Kongamano la Jumuiya ya Afrika Mashariki katika kuadhimisha Siku ya Mabunge Duniani, kuhusu suala la Makazi, lililofunguliwa leo Agosti 19, 2013 jijini Arusha.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki, wakati akiondoka baada ya kufungua rasmi Kongamano la Jumuiya ya Afrika Mashariki katika kuadhimisha Siku ya Mabunge Duniani, kuhusu suala la Makazi, leo Agosti 19, 2013 jijini Arusha.
Na Richard Mwangulube/ Arusha
Makamu wa Rais Dakta Mohammed Bilal leo, amefungua mkutano wa kwanza wa Makazi ulioandaliwa na Jumuiya ya afrika ya Mashariki (EALA) Mjini Arusha huku akisema suala la makazi mijini ni changamoto kubwa linalozikabili nchi za bara la Afika.
Makamu wa Rais amewambia wabunge zaidi ya 150 wanaoshiriki mkutano huo kwamba ili kukabiliana na changamoto hizo Serikali katika nchi za Bara la Afrika ni lazima ziwekeze raslimali nyingi katika suala la makazi mijini ili kukabiliana na chgangamoto ya kuwepo na makazi holela pamoja na mazingira duni.
Dakta Bilal amesisitiza umuhimu kwa nchi za bara la Afrika kuwa na mipango mizuri ya makazi ili kuwepo na mipangilio mizuri ya ujenzi, miundo mbinu na amewataka wabunge wanaoshiriki mkutano huo kuangalia mambo yaliyofanyika katika miaka 25 ya utekelezaji wa malengo ya Melenia (MDGs), kasoro zilizojitokeza wakati wa utekelezaji wake na miakakti ya kukabiliana nazo.
Aidha, Dakta Bilal amewataka wabunge hao kuacha kuwa wakosoaji katika Serikali zao tu bali ni lazima wasaidie kuwa wabunifu katika kuandaa mipango mizuri ya mipango miji.
Amesema suala la makazi mijini ni moja ya mahitaji muhimnu ya binadamu ambalo linahitaji mtazamo mzuri, uratibu wa karibu .Hata hivyo amesema hadi sasa katika karne ya 21 bado makazi mengi yamejengwa kwa nyumba za miti, udongo na kuezekwa kwa majani.
Dakta Bilal amesisitiza kuwa Serikali ya Tanzania imechukua hatua mbalimbali za kukabiliana na changamoto za mipango holela na ujenzi holela, ambapo pia kumekuwepo na kukosekana kwa huduma zote muhimu za upatikanaji wa majisafi na salama, hudua za afya na uduni wa mazingira.
Akizungumza katika mkutano huo Rais wa UN-Habitat Barani Afrika ambaye pia ni Spika wa Bunge la Afrika ya Mashariki Margaret Nantongo Zziwa amesema mipango duni,kukosekana kwa maji safi na salama, kukosekana kwa uwekezaji wa kutosha na msongamano wa makazi ni changamoto kubwa inazikabili nchi za bara la afrika pamoja na mazingira duni.
Spika Zziwa amesisitiza kwama bara la Afrika kamwe haliwezi kuw ana ushindani katika dunia kama watu wake wanaishi kwenye mazingira machafu na makazi duni
Amesema kama Jumuiya ya Afrika ya Mashariki ( EAC) ni yetu ni kuhakikisha inaboresha huduma mbalimbali zinazotolewa kwa watu wetu kwa kuwepo na makazi bora,na huduma nzuri za afya pamoja na upatikanaji wa maji safi na salama
Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi wa Tanzania Prof Anna Tibaijuka amesema suala la mazi mijini linahitaji utashi mkubwa wa kisiasa ili kukabiliana na chanagamoto mbalimbali.
Amesema asilimia 50 ya makazi barani Afrika haiku katika mpangilio mzuri hali ambayo inatokana na kukosekana kwa mipango mizuri ya mipango miji.
Amesema katika nchi za afrika hakuna mipango miji mizuri na kuwataka wananchi kuheshimu sheria hata hivyo nchi nyingi za afrika hazijawa na mipango miji mizuri ambapo watu wanadhani ujenzi wa miji ni sawa na ujenzi wa vijijini.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira James Daud Lembeli amesisitiza kuwa masuala ya ardhi hapa Tanzania ni mali ya Tanzania na sio Jumuiya ya Afria ya Mashariki.
Mbunge Lembeli amesisitiza kuwa suala la siasa lisichukue nafasi katika upangaji wa mipango miji katika nchi za Afrika.Hata hivyo amesema lipo tatizo la baadhi kutoheshimu sheria za mipango miji, kuvamia maeneo ya wazi na ambayo yanalindwa na Sheria.
Amesitaka Serikali kuhakikisha sheria za ardhi zinasimamiwa kwa nguvu zote na mamlaka husika bila kuingiliw ana wanasiasa.
No comments:
Post a Comment