TANGAZO


Tuesday, August 6, 2013

Kiongozi wa upinzani Burundi arejea nchini


Rwasa alitoroka Burundi baada ya uchaguzi wa mwaka 2010 akihofia maisha yake
Kiongozi rasmi wa upinzani na zamani akiongoza waasi nchini Burundi Agathon Rwasa ametoka mafichoni baada ya miaka mitatu ya kuwa nje ya nchi.
Alikanusha madai kuwa alikuwa anaishi katika nchi ya kigeni muda huo wote na kusema kuwa atagombea uchaguzi wa mwaka 2015
Bwana Rwasa alimaliza uasi wake mwaka 2009 lakini akatoweka kabla ya uchaguzi wa mwaka 2010 kufanyika akisema alihofia maisha yake.Maafisa wa serikali walimzuia kuhutubia wafuasi wake wakisema kuwa hana ruhusa kufanya hivyo , na kwa hivyo akahutubia waandishi wa habari nyumbani kwake.
Uchaguzi huo ulikuwa wa pili kufanyika tangu kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu miaka 12.
Aliambia BBC kuwa yeye anaunga mkono demokrasia hasa kwa kuwa uchaguzi mkuu unatarajiwa kufanyika mwaka 2015.
"Wakati wa silaha umekwisha,'' alisema.
alikanusha ripoti kuwa alikimbia nchi jirani ya Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo, akisema kuwa muda wote alikuwa nchini Burundi.
Hata hivyo alisema kuwa angali ana wasiwasi kuhusu usalama wake.
Rais Pierre Nkurunziza na Bwana Rwasa waliongoza makundi ya waasii wa Kihutu waliokuwa wanapigana dhidi ya jeshi lililokuwa na watu wengi wa kabila la wa Tutsi waliokuwa wachache,wakati wa vita vya wenyewe kwa wnyewe vilivuosababisha vifo vya watu laki tatu.
Chama cha Rwasa cha FNL kilikataa kumaliza uasi wakati makundi mengine yaliyokuwa yanapigana kuungana na kuunda serikali ya muungano iliyofuatiwa na uchaguzi wa mwaka 2005.

No comments:

Post a Comment