Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya Barclays kitengo cha wateja binafsi, Musa Kitoi akitoa maelekezo kwa washindi wa droo ya tatu ya maisha bomba na Barclays Golden Briefcase katika halfa ya kuwakabidhi zawadi washindi hao iliyofanyika katika tawi la Kinondoni leo, jiji Dar es Salaam .
Dkt.Kunda John akichagua mojawapo ya Golden Briefricase katika droo ya tatu ya Maisha bomba na Barclays ambapo aliibuka na ushindi wa Vocha yenye thamani ya sh 200,000 kwa ajili ya kufanya manunuzi ya vitu mbalimbali katika duka la Game.
Nabil Khan mmojawapo wa wateja wa Benki ya Barclays aliyeshinda Ipad 3 katika droo ya tatu ya maisha bomba na Barclays leo, jijini Dar es Salaam.
Martha Hewison akionesha karatasi ya ushindi wa mashine ya kufulia nguo katika droo ya maisha bomba na Barclays, Dar es Salaam leo.
Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya Barclays, Kitengo cha wateja binafsi, Musa Kitoi (wa kwanza kulia), akiwa katika picha ya pamoja na washindi wa droo ya tatu ya maisha bomba na Barclays Martha Hewison (wakwanza kushoto), aliyeshinda mashine ya kufulia nguo, Nabil Khan aliyeshinda Ipad 3, Darvish Bhatt na Kunda John waliojishindia vocha ya manunuzi katika duka la Game, leo jijini Dar es Salaam.
Eliuteri Mangi akichagua kuponi ya mshindi wa bahati nasibu ya maisha bomba na Barclays iliyofanyika katika tawi la Benki hiyo, Kinondoni leo, jijini Dar es Salaam.(Picha zote na Lorietha Laurence).
No comments:
Post a Comment