TANGAZO


Sunday, July 21, 2013

Ziara ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda Mjini Songe

IMG_0003 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa  Idara ya uhamiaji wakati alipowasili kwenye jengo la Idara hiyo mjini Songea kuweka jiwe la msingi akiwa katika ziara ya mkoa wa Ruvuma Julai 20, 2013.
IMG_0060 1 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua mabwawa ya kufugia samaki wakati alipotembelea Kituo cha Maendeleo  ya Ufugaji Samaki cha Ruhila kilichopo mjini Songea. Alikuwa katika ziara ya mkoa wa Ruvuma Julai 20, 2013. 
IMG_0087 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitazama chakula cha samaki wakati alipotembelea Kituo cha Maendeleo  ya Ufugaji wa Samaki cha Ruhila kilichopo Songea Mjini akiwa katika ziara ya mkoa wa Ruvuma Julai 20, 2013. Wapili kulia ni mkewe, Mama Tunu Pinda na Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Thabit Mwambungu. 
IMG_0163 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitazama moja  ya magari ya mafunzo  yanayotumika katika Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Tanzania  (VETA) cha Songea wakati alipokizindua,Julai 20, 2013. 
IMG_0194 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Mkewe Tunu (wapili kuhoto) wakitazama vyakula na vifaa mbalimbali vya jikoni katika maonyesho ya  kozi zinazofndishwa na Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Tanzania (VETA) cha Songea wakati alipokizindua Julai 2013. 
IMG_0219 
Wanachuo wa Chuo cha Mafunzo ya Elimu ya Ufundi  Tanzania (VETA) ambao majina hakupatikana wakionyesho mavazi yanayoshonwa na wanachuo wa Chuo hicho kabla ya mgeni rasmi Waziri Mkuu , Mizengo Pinda alipozindua Chuo chao mjini Songea Julai 20, 2013. Mheshimiwa Pinda alikuwa katika ziara ya mkoa wa Ruvuma.
IMG_0298 
Wairi Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Tunu wakisalimiana na madiwani wa Manispaa ya Songea wakati Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alipohutubia mkutano wa hadhara  mjini Songea akiwa kayia ziara ya mkoa wa Ruvuma Julai 20, 2013. 
IMG_0336 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  na mkewe Tunu (kushoto kwake) wakitazama ngoma ya wanawake wa Songea kabla ya kuhutubia mkutano wa hadhara mjini Songea Julai 20, 2013. 
IMG_0343
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Songea Girls baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara mjini Songea Julai 20, 2013.
IMG_0344 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Songea Girls baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara mjini Songea Julai 20, 2013. Alikuwa katika ziara ya mkoa wa Ruvuma.
IMG_0374 1 
Baadhi ya Waislamu wa Songea wakishiriki katika futari  wakati Waziri Mkuu, Mkuu Mizengo Pinda alipofuturisha kwenye Ikulu ndogo a  ya Songea akiwa katika  ziara ya mkoa wa Ruvuama Julai 20, 2013. 
IMG_0456 
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda  (wapili kulia)  akizungumza na baadhi ya wanawake  walioshiriki katika futari ambayo Waziri Mkuu, Mizengo Pinda aliwaandalia baadhi ya Waislam wa Songea Julai 20, 2013. Alikuwa katika ziara ya mkoa wa Ruvuma. (Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment