Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (katikati), akimkabidhi tuzo ya heshima ya udhamini wa maonesho hayo, Ofisa Masoko wa Nje wa Kampuni ya Tanzania Distilleries Limited (TDL), Babon Ndumati katika hafla hiyo.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (kulia) akimkabidhi tuzo Meneja Uhusiano Mambo ya Nje wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Emma Orio kwa kutambua mchango wa kampuni hiyo wa kufadhili sherehe za kufunga Maonesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Dar es Salaam leo.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (katikati), akimkabidhi tuzo ya ushindi wa jumla wa maonesho hayo, Meneja Kiongozi, Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Mfuko wa Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume katika hafla hiyo. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade), Sabetha Mwambenja, Waziri wa Viwanda na Biashara Dk. Abdallah Kigoda, Kaimu Mkurugenzi wa Tantrade, Jaqueline Maleko na Mkuu
wa Wilaya ya Temeke Sophia Mjema.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimkabidhi tuzo ya Sekta ya Habari na Mawasiliano, Meneja wa Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL),
Amini Mbaga katika hafla hiyo.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimkabidhi tuzo ya ushindi wa pili wa jumla wa maonesho hayo Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maeneo Maalumu ya Uwekezaji Tanzania (EPZA), Dk. Adelhelm Meru.
No comments:
Post a Comment