Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Joseline Kamuhanda (kushoto) na Meneja wa Red dot Tanzania, Nishad Mairal (katikati), wakimshuhudia Meneja Mauzo ya ziada wa Vodacom Tanzania, Liginiku Millinga, akiionesha modem yenye GB 6, Dar es Salaam leo, wakati wa hafla ya uzinduzi wa ushirikiano kati ya Red Dot na Vodacom, ambayo mteja atakayenunua kompyuta mpakato (laptop), aina ya DELL kwa bei nafuu atapata ofa ya modem hiyo bure kwa muda wa miezi miwili. (Picha zote na Mpigapicha wetu)
Na Mwandishi wetu, Dar es Salam
KATIKA kukidhi kasi ya maendeleo ya teknolojia kwa Watanzania hususani wanafunzi wa Vyuo na watu mbalimbali, Kampuni ya Vodacom kwa kushirikiana na Intel Tanzania wameungana na kutangaza ofa ya kompyuta mpakato (Laptop), itakayouzwa kwa bei nafuu pamoja na modem iliyounganishwa na intanet kwa miezi miwili.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla iliyofanyika katika banda la Vodacom kwenye maonesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam leo, Meneja wa Malipo ya kabla wa Vodacom Liginiku Milinga alisema kuwa mtu yeyote atakaye nunua kompyuta hiyo atazawadiwa modem yenye ya intanet yenye GB 6.
"Pindi mteja atakaponunua kompyuta hii atapewa modem yenye namba maalum ya Modem ambayo atatakiwa kuituma kwenda Vodacom na ataunganishwa moja kwa moja na huduma ya intanet kwa kupata GB 3 kwa miezi miwili mfurulizo,î
Milinga amesema Vodacom imekuwa mbele katika kuhakikisha inarahisisha maisha ya Watanzania ili kuwawezesha kukidhi mahitaji yao ya kila siku kwa kundana na kasi ya maendeleo ya sayansi na teknolojia.
ìDunia ya sasa imeshuhudia mapinduzi makubwa ya kiteknolojia laptop pamoja na internet vimekuwa vitendea kazi muhimu kwa kila mtu, tumeona vyema kuja na ofa hii ili kuwawezesha watanzania zaidi kuweza kumiliki Laptop kwa bei nafuu,î alisema milinga.
Aidha aliongeza kuwa ni vyema sasa wakati huu wanafunzi wanaotegemea kujiunga na vyuo mwakani kuchangamkia ofa hiyo ili kujiweka mahala pazuri zaidipindi watakapojiunga na vyuo kutokana na uhitji mkubwa wa vitendea kazi hivyo kwa wanafunzi wa vyuo.
Mbali ya hayo mteja atakae nunua kompyuta hizo anapata fursa ya kuingizwa kwenye droo kubwa ya sh.200,000 itakayokuwa ikifanyika mara moja kila mwezi iwapo mteja atatumia huduma ya M-pesa kufanyia manunuzi ya mahitaji mbalimbali.
No comments:
Post a Comment