TANGAZO


Monday, July 22, 2013

Rais Kikwete aongoza wananchi kuaga miili ya wanajeshi wa JWTZ waliofariki Darful nchini Sudan

Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza jambo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini, Meja Jenerali, Davies Mwamunyange, wakati wa hafla ya kuiaga miili ya wanajeshi saba wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), waliouawa Darful nchini Sudan. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Rais Jakaya Kikwete akisaini kitabu cha maombolezo ya wanajeshi saba wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), waliofariki Darful nchini Sudan, wakati wa hafla ya kuiaga miili yao, Dar es Salaam leo.  Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki na wapili kulia ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Shamsi Vuai Nahodha.
Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete, akisaini kitabu cha maombolezo.
Wanajeshi wakiteremsha moja ya majenenza yenye miili ya wanajeshi wenzao 7, waliofariki Darful nchini Sudani, wakati wa hafla ya kuwaaga, Dar es Salaam leo.

Baadhi ya wanajeshi na wananchi mbalimbali waliofika katika hafla ya kuiaga miili hiyo, wakifuatilia matukio mbalimbali yaliyokuwa yakitendeka viwanjani hapo.
Wanajeshi wakiteremsha moja ya majenenza yenye miili ya wanajeshi wenzao 7, waliofariki Darful nchini Sudani, wakati wa hafla ya kuwaaga, Dar es Salaam leo.
Baadhi ya wafiwa, wajane wa marehemu pamoja na marafiki wakiwa katika hafla hiyo.
Wanajeshi wakiliweka sehemu ya kuagia moja ya majenenza yenye miili ya wanajeshi wenzao 7, waliofariki Darful nchini Sudani, wakati wa hafla ya kuwaaga, Dar es Salaam leo.
Rais Jakaya Kikwete na mkewe, Mama Salma, wakitoa heshima zao za mwisho kwa mmoja wa mwili wa wanajeshi saba, waliouawa Darful nchini Sudan, wakati wakilinda amani nchini humo. Rais Kikwete alikuwa katika hafla ya kuiaga miili ya wanajeshi hao, Dar es Salaam leo.
Rais Jakaya Kikwete akiwapa mkono wa pole baadhi ya wafiwa na wajane wa wanajeshi hao, wakati wa hafla ya kuiaga miili yao, Dar es Salaam leo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd akiwapa pole baadhi ya wafiwa na wajane wa wanajeshi hao, wakati wa hafla hiyo leo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdurrahana Kinana, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana, wakiwapa pole wafiwa na wajane wa marehemu hao.
Mbunge Anna Abdallah, Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi, Profesa Sarungi na baadhi ya waombolezaji wakitoa heshima zao za mwisho kwa miili hiyo.
Baadhi ya wanajeshi wa JWTZ, wakitoa heshima zao za mwisho kwa miili hiyo, wakati wa hafla hiyo.

Baadhi ya wanajeshi wa JWTZ, wakiwapa pole wafiwa na wajane wa marehemu hao.
 
 
 Haya ni majeneza yaliyokuwa na miili ya marehemu hao.
 
 
 
 
 
 
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Meja Jenerali, Davies Mwamunyange, akielezea halihalisi ya tukio la mauaji ya wanajeshi hao, lilivyotokea Darful nchini Sudan, wakati wa hafla ya kuiaga miili yao jijini leo.
 

 
Amiri Jeshi Mkuu, Rais Jakaya Kikwete akihutubia wakati wa hafla hiyo huku akielezea masikitiko yake juu ya vifo hivyo pamoja na mambo mengine ya kufuatwa na Umoja wa Mataifa (UN) kwa ajili ya kuondoa kasoro zilizopo sasa na kuepusha majanga kama hayo katika kutekeleza jukumu la ulinzi wa amani kwa nchi zenye machafuko siku zijazo.


Wanajeshi wa Jeshi la Wanachi wa Tanzania (JWTZ), wakiwa wamelibeba moja ya jenenza lenye mwili wa mmoja wa wanajeshi saba wa Tanzania waliofariki Darful nchini Sudan, wakati wa kuiaga miili yao, Dar es Salaam leo.
 
Wanajeshi wa Jeshi la Wanachi wa Tanzania (JWTZ), wakiwa wamelibeba jenenza lenye mwili wa mmoja wa wanajeshi saba wa Tanzania waliofariki Darful nchini Sudan, wakati wa hafla hiyo.


Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa Umaja wa Mataifa, Dk. Asha-Rose Migiro, akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa hafla hiyo leo.
Magari yaliyokuwa yamebeba majenenza yenye miili ya askari waliofariki Darful yakiondoka kwenye eneo la kuagia, Makao Makuu ya Jeshi la Wananchi, Upanga Dar es Salaam leo kuelekea sehemu walizitokea.

No comments:

Post a Comment