TANGAZO


Saturday, July 20, 2013

Miili ya Askari wa JWTZ yawasili jijini Dar es Salaam tayari kwa mazishi

Miili ya askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ikiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, askari hao walikuwa wakilinda Aman Darfur Sudan. Miili hiyo itaagwa kwa heshima za kijeshi siku ya Jumatatu Julai 22 Makao Mkuu ya Wizara ya Ulinzi Upanga jijini Dar es Salaam.
Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiwa wamebeba moja ya masanduku saba yenye miili ya askari wa jeshi hilo waliofariki Darfur, Sudan wakati wakilinda amani, baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam leo alasiri.

No comments:

Post a Comment