TANGAZO


Monday, June 10, 2013

Wachimba migodi 55 Waafrika, Jela- Ghana


Wachimba migodi haramu watiwa nguvuni Ghana.
Polis nchini Ghana wamewatia nguvuni watu 55 raia wa nchi mbali mbali kutoka Afrika Magharibi wanaoshukiwa kuendesha shughuli haramu za uchimbaji haramu wa dhahabu, msemaji wa wizara ya uhamiaji ameambia BBC.
Kukamatwa kwao kunaashiria kuwa polisi wameelekeza nguvu zao sasa kwa wahamiaji wa Kiafrika kutoka kwa Wachina kama anavyo ripoti mwandishi wa BBC Akwesi Sapong akiwa nchini Ghana.
Serikali hiyo ya Ghana iliwaachilia washukiwa 124 raia wa Uchina wikendi na kuwaamuru waondoke nchini humo mara moja.
Sheria za Ghana zimeharamisha mwananchi yeyote wa kigeni kuajiriwa katika migodi midogo midogo ya nchi hiyo.
Ghana ndio nchi ya pili kwa uzalishaji mkubwa wa dhahabu barani Afrika baada ya Afrika Kusini.

Mwingilio wa Uchina

Kukamatwa kwa wageni imepokewa vizuri na raia wa Ghana masikini wanaoamini kuwa wafanyikazi kutoka nje wanadakia nafasi zao za ajira, kwa mujibu wa mwandishi wetu.
Msemaji wa wizara ya Uhamiaji Francis Palmdeti ameambia BBC kuwa kati ya 55 waliokamatwa, 51 ni raia wa Niger, 3 wametoka Togo na mmoj akutoka Nigeria.
'Bado uchunguzi unafanywa wa asili ya washukiwa wengine watatu baada wamedai kuwa raia wa Ghana na kukana kuwa wametoka Mali kama tulivyo shuku awali' amesema msemaji huyo.
Mwandishi wa BBC anasema kuwa oparesheni kama hii inamaanisha kuwa serikali imeazimia kumaliza uajiri wa mtu yeyote ambaye siye raia wa Ghana katika machimbo ya nchi hiyo.
Wachina watoa dhahabu Ghana
Washukiwa hao wamezuiliwa katika kituo cha Uhamiaji mjini Accra.
Kama anavyoarifu mwandishi wetu, serikali inapanga kuwahamisha washukiwa hao mara moja kinyume na kuwaachilia kama ilivyofanya wale raia wa Uchina kufuatia kuingilia kati suala hilo na ubalozi wa Uchina mjini Accra.
Duru kutoka kwa Ubalozi wa Uchina zinaarifu kuwa raia wao wengine 42 waliokamatwa awali katika machimbo manne tofauti wataachiliwa baadaye Jumatatu.
Mwandishi wetu anasema kuwa wachina walioachiliwa huru wameagizwa kuchukua ndege na kuondoka mara moja nchini humo.
Hata hivyo baadhi ya wafanyikazi wa kigeni wamedai kuwa wanazo hati halali kama wale wanaofanya kazi katika kampuni ya Honsol.
Kampuni hiyo ya Honsol inadai kuwa wakati wa msako uliofanywa na maafisa wa serikali katika afisi zake mwezi Machi, walipoteza dhahabu nyingi na mali yao nyingine kuharibiwa.
Wachina waliokamatwa Ghana.
Mnamo Oktoba mwaka uliopita kijana mmoja kutoka Uchina aliuawa katika msako kama huo dhidi ya wachimba migodi haramu.
Takriban wachina 100 pia walikamatwa katika mwezi huo huo wakidaiwa kuhusika na uchimbaji haramu.

No comments:

Post a Comment