Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel akionyesha msisitizo alipokuwa akiwasilisha mada kuhusu fikra za kibunifu kwa ajili ya kuinua uchumi kwa wanafunzi wa elimu ya juu leo jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Genofeva Matemu - MAELEZO)
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel akitoa mfano wa mabadiliko ya kiteknolojia kwa kutumia mfano wa Simu za mkononi leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wa mjadala kuhusu fikra za kibunifu kwa ajili ya kuinua uchumi kwa wanafunzi wa elimu ya juu wakifuatilia mada leo jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi kutoka Kampuni ya Breco inayojishughulisha na miradi ya kukamua Alizeti Kibaigwa Dodoma, Bi. Tatu Shamte akielezea kwa ufupi kuhusiana na kampuni hiyo wakati wa mjadala kuhusu fikra za kibunifu kwa ajili ya kuinua uchumi kwa wanafunzi wa elimu ya juu leo, jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mjadala kuhusu fikra za kibunifu kwa ajili ya kuinua uchumi kwa wanafunzi wa elimu ya juu leo jijini Dar es Salaam.
Na Frank Shija - MAELEZO
VIJANA wametakiwa kuwa wabunifu ili kujiletea maendeleo yao badala ya kusubiri kuajiriwa mara wanapomaliza masomo ya elimu ya juu.
Rai hiyo, imetolewa na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel, alipokuwa akiwasilisha mada kwa wanafunzi wa Elimu ya Juu wanaosoma masomo ya Sayansi kutoka Vyuo mbalimbali nchini, kuhusu fikra za kibunifu kwa ajili ya kuinua uchumi leo, jijini Dar es Salaam.
Aidha Prof. Gabriel amewataka vijana kuwa wabunifu ili kwenda na wakati ikiwa ni njia ya kukabiliana na changamoto na kasi ya mabadiliko ya kiteknolojia ambapo kila siku mambo yanabadilika kuendana na wakati.
“Pamoja na changamoto nyingi vijana mnapaswa kuwa wabunifu kwani ubunifu ndio njia pekee ya kushindana katika biashara na kuweza kukabiliana na kasi ya mabadiliko ya teknolojia katika maendeleo”, Amesema Prof. Gabriel.
Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa vijana wengi wamekosa uthubutu wa kujihusisha na ajira binafsi na kusababisha ongezeko la watu wasiokuwa na ajira kwani kwa sasa takwimu zinaonyesha kuwa kuna vijana takribani 16,195,370 nchini. Idadi hii ni sawa na 35.1% ambapo kati ya hao13.4% hawana ajira.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Kampuni ya Sparke International
inayojihusisha na bishara za kiwanda cha utengenezaji wa nguo, Bwana Gerald Reuben ambaye pia ni mwanafunzi wa elimu ya juu amesema kuwa wao kama vijana wamethubutu kujiajiri wenyewe na wanataraji kuajiri vijana wengi zaidi.
Reuben amesema kuwa Kampuni yao inatokana na muunganiko wa
vijana kutoka Chuo Kikuu Cha Dodoma kuunganisha mawazo na
kuanzisha Kampuni hiyo ambayo itasaidi wakulima wa zao la Pamba kuingia katika soko la ndani.
No comments:
Post a Comment