Kamati ya Bunge kuhusu maswala ya bajeti ya serikali, imekataa pendekezo la kuidhinisha pesa za kumnunulia rais Mstaafu Mwai Kibaki, ofisi ambayo itagharimu shilingi milioni miasaba za Kenya au dola milioni nane
Rais mstaafu alitengewa pesa hizo katika bajeti ya ziada iliyowasilishwa bungeni Jumanne wiki jana.
Wabunge hao waligundua kuwa ujenzi wa ofisi ulikuwa umetengewa pesa hizo walipohoji kwa nini hazina ya serikali ilikosa kutengewa shilingi bilioni 5.4 za ustawi wa maeneo bunge kwa kipindi cha mwaka 2012/2013
Walichojaribu kufanya katika bajeti hii ni kutumia pesa za maendeleo kwa miradi mingine ikiwemo ujenzi wa opfisi ya rais mstaafu.
Kamati hiyo pia iligundua kuwa moja ya mambo yaliyofanya na hazina ya serikali ni kutenga dola milioni nane kwa baraza na mawaziri kwa ununuzi wa jengo
Katibu wa baraza la mawaziri Francis Kimemia alitetea bajeti hiyo akisema kuwa ofisi inapaswa kununuliwa kwa ajili ya mikutano ya mawaziri.
Pia Kimemia alisema kuwa chini ya sheria, rais mstaafu anapaswa kuwa na ofisi, awe na katibu wake na wafanyakazi watakao simamia mipango yake kama alivyofanyiwa rais mstaafu Daniel Moi.
Kimemia aliambia shirika la habari na Nation nchini Kenya kuwa dola milioni nane ni pesa kidogo sana kwa ununuzi wa jengo lolote na kuwa alidhani kamati ingemwambia hizo ni pesa kidogo sana. Kimemia alisema hawana budi ila kumnunulia rais mstaafu ofisi kwa sababu hakuna jengo walilonalo kwa sasa kumkabidhi Kibaki.
Kimemia alisisitiza kuwa serikali imekuwa ikimtafutia ofisi yenye bei nafuu rais Kibaki mjini Niarobi kwani ofisi zote zilizopo sasa zinagharimu shilingi bilioni 1
No comments:
Post a Comment