Bunge la Ethiopia, limefutilia mbali mkataba uliosaniwa wakati wa utawala wa kikoloni, ulioipa Misri na Sudan, haki ya kutumia maji mengi ya mto Nile.
Serikali ya Ethiopia, imehoji kuwa mkataba huo ulioidhinishwa mwaka wa 1929, umepitwa na wakati.
Serikali ya Misri, imepinga vikali hatua hiyo na imekasirishwa na uamuzi wa Ethiopia wa kujenga bwawa la maji, katika mto huo wa Nile, ikidai kuwa itapunguza maji yake.
Siku ya Jumatatu rais Mohamed Morsi, alisema hataki vita, lakini anachunguza njia zote.
Awali, nchi sita zilizoko katika eneo la bonde la mto Nile, ikiwa ni pamoja na Ethiopia, zilisaini mkataba ambao unafutilia mbali mamlaka ya Misri ya kuzuia ujenzi wa bwana katika mto Nile.
No comments:
Post a Comment