Rais wa kwanza mweusi Afrika Kusini Mzee Nelson Madiba Mandela ameendelea kusalia Hospitalini kwa siku ya pili tangu alipolazwa hapo jana kutokana na matatizo ya mapafu yaliyoathiri mfumo wake wa upumuaji.
Maombi yamefanyika leo katika makanisa mbalimbali nchini Afrika kusini kumuombea afuweni Mzee Mandela anayeendelea kupokea matibabu hospitalini mjini Pretoria.
Taarifa kutoka ikulu inaeleza kwamba Bwana Mandela ambaye ana umri wa miaka 94 anapumua mwenyewe pasi usaidizi wowote.
Anaumwa mno lakini hali yake inaimarika,Alisema msemaji wa Mzee Mandela.
Rais Jacob Zuma ameashiria kwamba atamtembelea Mandela punde tu madaktari watakapotoa ruhusa.
Hii ni mara ya tatu kwa Mzee Mandela kulazwa hospitalini katika muda wa mizezi sita iliyopita.
Msemaji wa chama tawala cha ANC,Keith Khoza amesema anamini Mzee Mandela atapona.
No comments:
Post a Comment