Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya Chama cha Ukombozi cha Palestina (PLO), Tayseer Khalid, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika ofisini kwa makamu, Ikulu jijini Dar es Salaam jana, Juni 14, 2013.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa Chama cha Ukombozi cha Palestina (PLO) na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Dk. Asha-Rose Migiro wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wakiwa katika picha ya pamoja na ujumbe huo, mara baada ya mazungumzo jijini jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya Chama cha Ukombozi cha Palestina (PLO), Tayseer Khalid, baada ya mazungumzo yao, yaliyofanyika ofisini kwa makamu, Ikulu jijini Dar es Salaam jana, Juni 14, 2013. Kushoto ni aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Dk. Asha-Rose Migiro wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kulia ni Jihad Abu Zneid wa PLO.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Dk. Asha-Rose Migiro wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), baada ya mazungumzo hayo na Ujumbe wa Palestina yaliyofanyika ofisini kwa makamu, Ikulu jijini Dar es Salaam jana, Juni 14, 2013. Katikati ni Jihad Abu Zneid wa PLO.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akimkaribisha Waziri wa Ulinzi wa Comoro, Hamada Madi, wakati alipofika ofisini kwake, Ikulu jijini Dar es Salaam jana, Juni 14, 2013 kwa ajili ya kumkabidhi Ujumbe maalum wa Serikali ya watu wa Comoro. Makamu alipokea ujumbe huo kwa niaba ya Rais Jakaya Kikwete.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akipokea Ujumbe maalum kutoka kwa Waziri Ulinzi wa Comoro, Hamada Madi, aliyefika ofisini kwa makamu, Ikulu jijini Dar es Salaam jana, Juni 14, 2013 kwa ajili ya kumkabidhi ujumbe maalum wa Serikali ya watu wa Comoro. Makamu alipokea ujumbe huo, kwa niaba ya Rais Jakaya Kikwete.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Waziri wa Ulinzi wa Comoro, Hamada Madi, wakati alipofika ofisini kwake, Ikulu jijini Dar es Salaam jana, Juni 14, 2013 kwa ajili ya kumkabidhi ujumbe maalum wa Serikali ya watu wa Comoro. Makamu alipokea ujumbe huo, kwa niaba ya Rais Jakaya Kikwete.
No comments:
Post a Comment