TANGAZO


Saturday, June 15, 2013

Iran yapata rais mpya

Hassan Rouhani

Kiongozi wa chama chenye msimamo wa Kimhafidhina nchini Iran, Hassan Rouhani, ametangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais nchini Iran.
Wizara ya mambo ya ndani nchini humo imesema, Bwana Rouhani ameshinda za zaidi ya kura millioni kumi na nane, ambayo ni zaidi ya asilimia hamsini ya kura zote zilizopigwa.
Wizara hiyo imesema kuwa, idadi kubwa ya raia wa nchi hiyo walijitokeza kupiga kura kiwango ambacho kinakadiriwa kuwa asilimia sabini na tatu ya watu waliosajiliwa.
Mayor wa mji wa Tehran, Mohamad Baqar Qalibaf, alimaliza katika nafasi ya pili.

No comments:

Post a Comment