Hali ya Afya ya aliyekuwa rais wa Afrika Kusini Nelson Mandela, inaendelea kuimarika.
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma, amesema kuwa amefahamishwa na madaktari wanaomtibu kuwa, hali ya Mzee Mandela ambaye anaendelea kupokea matibabu katika hospitali moja mjini Pretoria imeimarika.
Rais Zuma amesema amefurahishwa na jinsi hali ya rais huyo inavyoendelea kuimarika, baada ya kudhohofika sana siku chache zilizopita.
Siku ya Jumanne rais Zuma, alisema kuwa nchi yote inazidi kumwombea Mzee Nelson Mandela ili apate afueni haraka.
Rais huyo wa zamani amelazwa hospitalini Pretoria, ambako anatibiwa maambukizi ya mapafu.
Katika taarifa yake rais Zuma amesema japokuwa Mandela ameathirika sana, madaktari wanaomshughulikia wanafanya kazi nzuri.
Rais huyo mstaafu wa Afrika Kusini, amelazwa hospitalini kwa siku ya tano leo ambako anapokea matibabu ya ugonjwa wa mapafu.
Duru kutoka kwa ofisi ya rais Jacob Zuma, zinasema kuwa Mandela mwenye umri wa miaka 94, yuko katika hali mbaya ingawa imeweza kudhibitiwa.
Familia ya Mandela
Jamaa zake pamoja na aliyekuwa mkewe Winnie Madikizela-Mandela, walimtembelea hospitalini Jumatatu
Mwanawe Mandela Zenani (Mandela-Dlamini), pia alirejea kutoka nchini Argentina, ambako yeye ni balozi.
Serikali imekuwa ikisema kuwa hali ya Mandela inatia wasiwasi ingawa madaktari wameweza kuidhibiti.
Amekuwa katika chumba ya wagonjwa mahututi tangu kulazwa hospitalini Jumamosi kwa mara ya tatu mwaka huu.
Mwezi Disemba , bwana Mandela alilazwa hospitalini kwa siku 18 baada ya kupata maradhi ya mapafu,
Kumekuwa na taarifa za simanzi kwa mara ya kwanza huku familia yake ikikusanyika kando yake, baadhi ya watu wakisema kuwa ni muda wamwache Mandela aende zake.
Bwana Mandela, mwenye umri wa miaka 94, alipelekwa hospitalini mapema Jumamosi , ikiwa ni mara ya tatu kulazwa hospitalini mwaka huu.
Kwa mujibu wa duru za urais, Mandela amekuwa akiugua kwa muda mjini Johannesburg baada ya kukumbwa tena na ugonjwa wa mapafu.
Msemaji wa serikali Mac Maharaj amesema kuwa maafisa katika hospitali wanataka kudhibiti idadi ya watu wanaozuru hospitali hiyo ili wampunguzie bwana Mandela usumbufu.
Alilazwa hospitalini baada ya hali yake kuwa mbaya zaidi mnamo Jumamosi.
Kwa mujibu wa taarifa za urais, Rais Jacob Zuma, amerejelea wito wake kwa watu nchini Afrika Kusini kumuombea Madiba wakati huu anapougua.
Lakini mwandishi wa BBC mjini Pretoria, Karen Allen, anasema kuwa kuna matumaini madogo kuwa Mandela aliyeongoza vita dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi, huenda akapona.
Anasema kuwa wengi walipata matumani baada ya bintiye Mandela Zindzi, kusema kuwa babake yuko salama na kuwa anaendelea kupata nafuu.
Mkewe Mandela Graca Machel, alifutilia mbali, ziara yake mjini London Jumamosi ili kuwa kando ya mumewe.
Mandela alikuwa Rais wa Afrika Kusini kati ya mwaka 1994 hadi 1999.
Alifungwa jela miaka 27 na anaaminika kuwahi kuugua ugonjwa wa mapafu alipokuwa akifanyishwa kazi ngumu katika machimbo ya mawe akiwa jela.
No comments:
Post a Comment