TANGAZO


Friday, May 17, 2013

Vita vyashika kasi dhidi ya Boko Haram



Operesheni ya kijeshi imeanza dhidi ya Boko Haram ingawa wadadisi wanasema imekuja kuchelewa
Amri ya kutotoka nje usiku imetangazwa katika jimbo la Adamawa nchini Nigeria.
Jimbo hilo limeungana na mengine mawili ya kaskazini mashariki ya, Borno na Yobe, ambako serikali inasema kuwa wanajeshi wameanza oparesheni kubwa dhidi ya wapiganaji wa kiislamu wa kundi la Boko Haram .
Rununu hazikuwa zifanya kazi katika baadhi ya sehemu za eneo hilo.
Maafisa wa serikali wameiambia BBC kuwa ndege za kivita huenda zikapelekwa katika oparesheni.
Walisema kuwa wanajeshi walishambulia sehemu za jimbo la Borno, ambako kundi la Boko Haram lina ngome zake.
Operesheni hiyo inakuja baada ya serikali kutangaza hali ya hatari katika majimbo ya Borno, Yobe na Adamawa Kaskazini Mashariki mwa nchi ambako watu 2,000 yatari wameuawa tangu mwaka 2009.
Amri ya kutotoka nje kuanzia saa za jioni hadi asubuhi imetangazwa katika jimbo la Adamawa ili kukabiliana na wanamgambo hao.
Mwandishi wa BBC katika jimbo la Adamawa anasema kuwa uamuzi huo unashangaza kwani hali ya usalama katika jimbo hilo sio mbaya ikilinganishwa na majimbo ya Borno na Yobe.
Mnamo siku ya Alhamisi wanajeshi walivamia kambi za wanamgambo katika mbuga ya wanyama na ambayo inasifika kuwa moja ya ngome kuu za kundi la Boko Haram
Msemaji wa jeshi la Nigeria Brigedia Generali Chris Olukolade, alisema kuwa watatumia uwezo wao wote wa kijeshi kukabiliana vilivyo na wapiganaji wa Boko Haram.

No comments:

Post a Comment