Maafisa wa Uchina wameanzisha uchunguzi juu ya afisa wa ngazi ya juu katika kile kinachoonekana kama hatua ya hivi karibuni ya kiongozi wa nchi hiyo Xi Jinping ya kukabiliana na ufisadi.
Katika ripoti fupi iliyotolewa na serikali ya Uchina kupitia shirika la habari la uchina Xinhua imesema kuwa Liu Tienan - mkuu wa sera za uchumi - alisimamishwa kazi baada ya kushutumiwa kukiuka vikali nidhamu.
Hii ni kesi ya kwanza kwa afisa wa ngazi ya juu wa uchina kutolewa hadharani tangu mwaka jana baada ya mwandishi wa habari wa kichina kumshutumu wazi Bwana Liu kwa ufisadi , kugushi vyetii vyake vya elimu na kutishia kumuua hawara wake .
Nchini Uchina ambako vyombo vya habari vinabanwa , shutuma hizi ni kubwa dhidi ya afisa wa ngazi ya juu. Lakini sasa maafisa wanasema bwana Liu anachunguzwa , licha ya kwamba hawakueleza bayana anakabiliwa na shutuma gani hasa .
Tangu aingie mamlakani Rais Xi Jinping - aliapa kukabiliana na ufisadi , akionya kuwa ni tisho kwa utawala wa chama chake cha kikomunisti .
Uchunguzi huu utaangaliwa kama jaribio kwa rais mpya la kuweza kushawishi umma kuwa anaweza kweli kumaliza uhalifu huo
No comments:
Post a Comment