Askofu mstaafu wa Cape Town, Afrika Kuisni, Desmond Tutu, amesema hatapigia kura tena ANC, chama tawala cha nchi hiyo.
Katika makala aliyoandika kwenye magazeti ya Mail na Guardian, Desmond Tutu, aliyepewa tuzo ya Nobel ya amani, alisema ANC iliongoza vema vita vya ukombozi lakini haikufanikiwa kuwa chama cha kisiasa.
Alitoa mfano wa tofauti baina ya maskini na matajiri, fujo na rushwa kuwa sababu zinazomfanya kuacha kuunga mkono chama hicho.
Zamani Desmond Tutu alikuwa mfuasi mkubwa wa chama hicho lakini katika miaka ya karibuni amekilaumu kwamba hakikushughulikia watu wa kawaida.
No comments:
Post a Comment