Mabingwa wa Ligi Kuu nchini Uingereza, Premier League
,Manchester United, wametangaza kwamba, Sir Alex Ferguson atastaafu kama meneja
wa klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu.
Sir Alex anatajwa kuwa ndiye meneja mwenye mafanikio makubwa katika historia
ya soka la Uingereza.Tangu alipojiunga na klabu hiyo mnamo mwaka 1986, ameshinda mataji mawili ya Klabu Bingwa Barani Ulaya, mataji kumi na tatu ya Ligi Kuu na Kombe la FA mara tano.
Katika taarifa yake, Sir Alex amesema ni muda muafaka kwake kustaafu wakati klabu ikiwa imejizatiti katika nafasi nzuri. Atabakia Manchester United kama mmoja wa wakurugenzi na balozi.
No comments:
Post a Comment