TANGAZO


Monday, May 6, 2013

Simba ilivyoipiga Ruvu Shooting mabao 3-1 Ligi Kuu ya Vodacom, Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam

Haruna Chanongo (kushoto) wa Simba, akiwania mpira na Michael Pius wa Ruvu Shooting FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, uliochezwa Uwanja wa Taifa Dar es Salaam jana jioni. Katika mchezo huo, Simba imeifunga Ruvu mabao 3-1. (Picha zote na Kassim Mbarouk)

Haruna Chanongo wa Simba, akimtoka Michael Pius wa Ruvu Shooting FC katika mchezo huo.

Felix Sunzu wa Simba akiwania mpira na Ernest Ernest wa Ruvu Shootings FC katika mchezo huo.

Felix Sunzu wa Simba akimzidi nguvu Ernest Ernest wa Ruvu Shootings FC na hivyo kuudhibiti mpira huo.

Wachezaji wa Simba wakishangilia bao la kwanza la timu hiyo, lililofungwa na Amri Kiemba kwa staili ya aina yake (kusujudu), wakati wa mchezo dhidi ya Ruvu Shootings.

Wachezaji wa Simba, wakimpongeza Amri Kiemba baada ya kuifungia timu yake hiyo bao la kwanza dhidi ya Ruvu Shootings FC.

Mashabiki wa Simba wakishangilia bao la kwanza la timu hiyo, lililofungwa na Amri Kiemba kwa shuti la mbali alilolipiga akiwa nje ya mita 18.

 Felis Sunzu wa Simba akiwa amedondoshwa chini na Nyambiso Athuman wa Ruvu Shootings FC.

 Haruna Chanongo wa Simba, akiwania mpira wa juu na Michael Pius wa Ruvu Shooting FC katika mchezo huo.
Wachezaji wa Ruvu Shooting FC, wakipongezana baada ya mchezaji Abdulrahaman Mussa kuisawazishia goli timu yake kabla ya timu hiyo kumiminiwa mabao mengine mawili na Simba SC na hivyo Simba kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 katika mchezo huo.

Ubao wa matangazo ukionesha Simba 1 na Ruvu Shootings 1, wakati huo.

No comments:

Post a Comment