TANGAZO


Thursday, May 9, 2013

Sheikh Ponda na wenzake 49 waachiwa huru, afungwa kifungo cha nje mwaka mmoja

Askari Polisi akitaja majina ya walioshitakiwa pamoja na Sheikh Ponda kwa ajili ya kuwapanga vizuri kabla ya kutolewa hukumu kwenye Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam leo. (Picha zote na Khamisi Mussa)


Askari Magereza akimvua pingu Katibu wa Taasisi na Jumiya za Kiisalamu, Sheikh Ponda Issa Ponda Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam leo, wakati alipofikisha mahakamani hapo kwa ajili ya kusikiliza hukumu ya kesi yake iliyokuwa ikimkabili.

Askari wakiwa kwenye msafara wa kumsindikiza Sheikh Ponda Issa Ponda mara baada ya kuachiwa huru na Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam leo na mahakama hiyo, kumpa kifungo cha nje ambapo ametakiwa kutokujihusisha na kuhamasisha vurugu na fujo kwa kipindi cha mwaka mmoja (miezi 12).

Sheikh Ponda akiswali katika Msikitini wa Mtambani, Kinondoni jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kuachiwa huru na Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam.


Wafuasi wa Sheik Ponda Issa Ponda, wakimshangilia alipokuwa akihutubia ndani ya Msikiti wa Mtambani jijini Dar es Salaam leo.

Katibu wa Jumuia za Taasisi za Kiisalamu Tanznania, Sheikh Ponda Issa Ponda akifanya mahubiri katika Msikitini wa Mtambani, Kinondoni Dar es Salaam, alipokwenda leo baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kumwachia huru, yeye na wenzake 49, waliokuwa wanakabiliwa na shitaka la uchochezi.

No comments:

Post a Comment