TANGAZO


Wednesday, May 29, 2013

Polisi Kenya watuhumiwa kuwatesa wakimbizi



Mtafiti mkuu wa shirika la HRW Gerry Simpson
Polisi nchini Kenya wametuhumiwa kwa kuwabaka na kuwazuilia kiholela takriban wakimbizi 1,000, huku wakijidai kupambana na ugaidi.
Kwa mujibu wa shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch, polisi kutoka vikosi vinne waliwadhulumu wakimbizi wa kisomali na wa Ethiopia pamoja na watu wengine waliokuwa wanatafuta hifadhi nchini Kenya katika mtaa wa Eastleigh, mjini Nairobi kati ya Novemba na Janurai mwaka jana.
Walioshuhudia vitendo hivyo pamoja na wakimbizi wenyewe, waliambia shirika la HRW, kuwa polisi wa kikosi cha GSU, wa kupambana na ghasia, polisi wa kawaida na wale wa utawala pamoja na maafisa wa ujasusi, walifanya vitendo hivyo.
Inasemekana kuwa waliwadhulumu, kuwabaka, kuwapora , kuwachapa na kuwakamata wakimbizi kiholela na kisha kuwazuilia katika mazingira ya kinyama.
Ripoti hiyo yenye madai ya karibu wakimbizi 101 waliohojiwa, ilisema kuwa wanawake na watoto ni miongoni mwa waathiriwa.
Mtafiti mkuu wa shirika hilo,Gerry Simpson, alisema kuwa maafisa wa utawala nchini Kenya wanapaswa kuanzisha uchunguzi huku shirika la kuwahudumia wakimbizi la UNHCR ambalo halijatamka lolote hadharani kuhusu vitendo hivyo, nalo likijitahidi kurekodi na kuvilaani visa vya dhuluma dhidi ya wakimbizi

Polisi wa GSU wakifanya msako katika moja ya mitaa mjini Nairobi
"wakimbizi walitusimulia kuhusu namna ya mamia ya polisi walivyowatendae unyama jamii zao kwa wiki kumi na hata kuwaibia miongoni mwao walio maskini zaidi,'' alisema afisaa huyo wakati wa kutangaza ripoti hiyo.
Bwana Simpson alisema kuwa wakimbizi 96 ambao wamesajiliwa, walisimulia ambvyo polisi walifanya msako katika nyumba zao nyakati za usiku.
Kwa mujibu wa shirika hilo, wakimbizi pamoja na wakenya wenye asili ya kisomali, walikumbwa na dhuluma hizo kutoka kwa maafisa wa usalama waliowatuhumu kuwa magaidi.
Shirika hilo linataka wakuu wa polisi kuamuru polisi kuacha vitendo vya kuwahangaisha wakimbizi pamoja na kukomesha vitendo vya ubakaji, na mateso mengine wanayowafanyia wakimbizi.

No comments:

Post a Comment