Baadhi ya ndugu wa marehemu Vicky Mgoyo, wakiwa nyumbani kwao kulikofanyika shughuli za maziko kabla ya kuupeleka Kanisa la KKKT, Usharika wa Kibangu kwa maombezi na kisha kupelekwa shambani kwake, Mapinga kwa mazishi leo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Jambo Concepts wakiwa nyumbani kwa marehemu mfanyakazi mwenzao, Vicky Mgoyo leo.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Jambo Concepts, inayochapisha magazeti ya Jambo Leo, jarida la Jambo Brand, Staa Spoti na Dar Metro, Juma Pinto (katikati) na mmoja wa Wakurungenzi wa kampuni hiyo, Benny Kisaka (kulia), wakimliwaza mtoto mkubwa wa aliyekuwa Mhasibu Mkuu wa kampuni ya Jambo Concepts, Vicky Mgoyo, Muhere Mgoyo, wakati wa shughuli za maziko, nyumbani kwa marehemu, Ubungo Kibangu, Dar es Salaam leo.
Mmoja wa watoto wa marehemu Vicky Mgoyo, Gati (wa pili kushoto), akisaidiwa na waombolezaji kupelekwa kwenye gari tayari kuelekea kanisani kwa sala na maombezi ya mwili wa mama yake huyo.
Waombolezaji wakiwa wamelibeba jenenza lenye mwili wa marehemu Vicky Mgoyo, kuliingiza kanisani kwa ajili ya misa ya kuuombea kabla ya shambani kwake Mapinga mkoani Pwani kwa mazishi leo.
Watoto wa marehemu Vicky Mgogoyo, Gati (kushoto), James (katikati) na Muhere Mgoyo (kulia), wakiwa katika hafla ya misa ya kuuombea mwili wa mama yao huyo katika kanisa hilo.
Watoto wa marehemu Vicky Mgogoyo, Muhere Mgoyo (kulia) na James wakiwa katika hafla ya misa ya kuuombea mwili wa mama yao huyo katika kanisa hilo.
Baadhi ya wafiwa wakiwa katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Ubungo Kibangu, wakati wa misa ya kuuaga mwili wa marehemu Vicky Mgoyo.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Jambo Concepts, Juma Pinto (kushoto), akiwa pamoja na mmoja wa Wakurungenzi wa kampuni hiyo, Benny Kisaka (kulia) na Meneja Biashara, Juma Mabakila, wakati wa misa ya kumuombea aliyekuwa Mhasibu Mkuu wa kampuni hiyo, Vicky Mgoyo katika kanisa la KKKT, Ubungo Kibangu, jijini Dar es Salaam leo.
Mtoto mkubwa wa aliyekuwa Mhasibu Mkuu wa Kampuni ya Jambo Concepts, Vicky Mgoyo, Muhere Mgoyo, akiuaga mwili wa mama yake katika Kanisa hilo, kabla ya kupelekwa shambani kwake, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, kijiji cha Mapinga kwa mazishi.
Jenenza lenye mwili wake likiwa kanisani hapo.
Mwili wa marehemu Vicky Mgoyo |
Mhariri Mkuu wa gazeti la Jambo Leo, Anicetus Mwesa (kulia), akiuaga mwili wa marehemu Vicky Mgoyo.
Mtoto mkubwa wa aliyekuwa Mhasibu Mkuu wa Kampuni ya Jambo Concepts, Vicky Mgoyo, Muhere Mgoyo, akiuaga mwili wa mama yake katika Kanisa hilo, kabla ya kupelekwa shambani kwake, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, kijiji cha Mapinga kwa mazishi.
Mtoto mkubwa wa aliyekuwa Mhasibu Mkuu wa Kampuni ya Jambo Concepts, Vicky Mgoyo, Muhere Mgoyo, akiuaga mwili wa mama yake katika Kanisa hilo, kabla ya kupelekwa shambani kwake, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, kijiji cha Mapinga kwa mazishi. Kushoto ni Mchungaji Richard Ananja wa Kanisa hilo.
Watoto wa marehemu Vicky Mgogoyo, Gati (kushoto) na James, wakiwa katika hafla ya misa ya kuuombea mwili wa mama yao huyo katika kanisa hilo leo.
Mtoto wa pili wa marehemu Vicky Mgoyo, James, akiwa ameubeba msalaba wa mama yake huyo kuanza kuelekea safari ya kwenda kuuzika mwili wake, kijijini Mapinga.
Waombolezaji wakiwa wamelibeba jenenza lenye mwili wa aliyekuwa Mhasibu Mkuu wa Kampuni ya Jambo Concepts, inayochapisha magazeti ya Jambo Leo, jarida la Jambo Brand, Staa Spoti na Dar Metro, Vicky Mgoyo, mara baada ya misa ya kuuombea iliyofanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Ubungo Kibangu, kuelekea kwenye mazishi yake, shambani kwake nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, kijiji cha Mapinga, mkoani Pwani.
No comments:
Post a Comment