Mfanyabiashara wa maji ya kunywa kwenye chupa, aliyetambulika kwa jina la Kigira Mhisho(15), akimwaga maji baada ya kubainika na wananchi kuwa anauza maji bandia, Mtaa wa Samora karibu na mzunguko wa Sanamu ya Askari, maeneo ya Posta, jijini Dar es Salaam leo. (Picha zote na Frank Shija - MAELEZO)
Wananchi wakimuhoji mfanyabiashara huyo, aliyekuwa akiuza maji feki leo, jijini Dar es Salaam.
Wananchi wakifuatilia mzozo baina ya mfanyabiashara wa maji hayo na mteja wake baada ya kubainika kwamba amemuuzia maji bandia. Mfanyabiashara huyo, aliyetambulika kwa jina la Kagira Mhisho, mwenye umri wa miaka 15, inasemekana kuwa amekuwa akifanya biashara hiyo kwa kutumia maji kutoka sokoni Kariakoo kwa takribani miaka mitatu sasa.
Tahadhari: Nivyema wananchi wakajihadhari na maji yanayouzwa njiani kwani baadhi ya wafanyabiashara wasiowaaminifu huokota chupa zilizokwisha tumika na kuzitumia kwa kuweka maji kwa njia wanazozifahamu wenyewe.
Watu hao wasiokuwa waaminifu, hujipatia fedha kwa kuwauzia wananchi maji yasiyo salama na yanayohatarisha afya zao.
Kwa upande wetu, tunavishauri vyombo husika katika ukaguzi wa bidhaa salama na bora za viwandani pamoja na wahusika wengine kuanza kufuatilia biadhaa mbalimbali zinazouzwa mikononi kwa ajili ya kuwakinga raia na athari za kiafya ambazo zinaweza kuwapata watumiaji (wananchi) wa bidhaa hizo holela.
Hii ni Rai ya Mtendaji Mkuu bayana.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment