Waandhishi wa habari, wakimsikiliza Rais wa Chama cha Wauguzi Tanzania (TANNA), Paul Magesa wakati alipokuwa akizungumza nao, Dar es Salaam leo, kuhusu maadhimisho ya Siku ya Wauguzi duniani itakayoadhimishwa Kitaifa nchini mkoani Rukwa, Mei 12, mwaka huu.
Rais wa Chama cha Wauguzi Tanzania (TANNA), Paul Magesa akizungumza na waandishi wa habari (kulia), Dar es Salaam leo, kuhusu maadhimisho ya Siku ya Wauguzi duniani itakayoadhimishwa Kitaifa nchini mkoani Rukwa, Mei 12, mwaka huu.
Waandhishi wa habari, wakiandika habari zilizokuwa zikitolewa na Rais wa Chama cha Wauguzi Tanzania (TANNA), Paul Magesa wakati alipokuwa akizungumza nao, Dar es Salaam leo, kuhusu maadhimisho ya Siku ya Wauguzi duniani itakayoadhimishwa Kitaifa nchini, mkoani Rukwa Mei 12, mwaka huu.
Na: Eliphace Marwa – Maelezo
07-05-2013
CHAMA cha Wauguzi Tanzania kimesema kuwa vifo vya mama wajawazito pamoja na watoto vimepungua sana nchini kutokana na kuboreshwa na kufikishwa kwa huduma muhimu kwa walengwa.
Kauli hiyo imetolewa na Rais wa chama hicho, Paulo Magesa wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam juu ya Maadhimisho ya Siku ya Waaguzi Duniani yatakayofanyika Mei 12 mwaka huu.
Magesa alisema maadhimisho hayo yanayotarajiwa kufanyika kitaifa mkoani Rukwa, yatakuwa na kauli mbiu inayosema kuwa “Kuziba pengo kufikia Malengo ya Milenia namba 6,5,4”.
Alisema kuwa malengo hayo ya millennia yanalenga kuzuia vifo vya kinamama wajawazito wakati wa kujifungua, kuzuia vifo vya watoto wenye umri chini ya miaka mitano na kuzuia maambukizi ya Virusi Virusi UKimwi(VVU) kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.
“Pamoja na changamoto nyingi tunazokutana nazo wauguzi bado tunajitahidi kwa kadri ya uwezo wetu kuhakikisha na hii imeleta mafanikio makubwa kwani”, alisema Magesa.
Alifafanua kuwa pamoja na changamoto nyingi wanazokutana nazo wauguzi nchini, bado wanajitahidi kwa kadri ya uwezo wao kuhakikisha huduma bora zinawafikia walengwa na hilo limeleta mafanikio makubwa.
Katika kuzuia na kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto nchini chini ya mpango wa Milenia,Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imelenga kuhamasisha akina mama kutumia njia salama za uzazi wa mpango na kuhakikisha wanajifungulia kwenye vituo vya kutolea huduma za mama na mtoto.
Katika maadhimisho hayo kutakuwa na maonesho kuanzia Mei 10 hadi Mei 12, kuonesha shughuli mbalimbali za kitaaluma wanazozifanya wauguzi ikiwa ni pamoja na kutoa huduma mbalimbali za kiafya kama huduma ya mama na mtoto, huduma za kupima VVU na ushauri nasaha.
Chama cha wauguzi Tanzania (TANNA) ni chama kinachowawakilisha wauguzi na wakunga wote Tanzania bara na Katika maadhimisho hayo Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Hussein Mwinyi.
No comments:
Post a Comment