Rais Goodluck Jonathan amekubali kuwa baadhi ya sehemu za nchi haziko chini ya udhibiti wa serikal
Msemaji wa Rais Good Luck Johnthan wa Nigeria amesema hatua ya kutangaza hali ya hatari katika majimbo matatu kaskazini mwa nchi, ni kuzuia taifa hilo dhidi ya kutumbukia kwenye vita.
Msemaji huyo Davip Okupi ameambia BBC kwamba magavana wa majimbo ya Borno, Yobe na Adamawa wameunga mkono mipango ya sasa, ili kukabiliana na mashambulio yanayotekelezwa na wapiganaji wa kiisilamu wa Boko Haram.
Akilihutubia taifa kupitia Runinga, Rais Good Luck Jonathan alisema serikali itatumia kila mbinu kumaliza kundi hilo.
Aliongeza kuwa wanamgambo walio na agenda ya kufanya mauaji ya halaiki, wametangaza vita nchini Nigeria.
Rais kwa mara ya kwanza amekubali kuwa sehemu kadfhaa za nchi haziko chini ya udhibiti wa serikali.
No comments:
Post a Comment