Mtangazaji wa kituo cha televisheni cha ITV, Rehema Salim (kulia), akiuliza kuhusu Akaunti ya Malkia kwa Ofisa Masoko wa Benki ya CRDB, Emmanuel Kiondo, mbele ya banda la benki hiyo wakati wa maonesho yaliyoambatana na Kongamano la Wajasiriamali Wanawake Tanzania, lililofanyika jana chini ya udhamini wa CRDB kupitia Malkia Akaunti.
Ofisa Masoko wa CRDB, Emmanuel Kiondo, akifanunua jambo kwa Rehema Salim kuhusu akaunti ya Malkia.
Emmanuel Kiondo, akitoa mada katika Kongamano la Wanawake, lililofanyika jijini Dar es Salaam jana. Katika kongamano hilo lililodhaminiwa na Benki ya CRDB kupitia Malkia Akaunti, Kiondo aliwasilisha mada isemayo 'Namna gani unaweza kuwekeza fedha zako' ikiwaelimisha wajasiriamali wanawake nia sahihi za uwekezaji fedha kwa maendeleo yao kibiashara, kielimu na kimaisha.
Ofisa Udhibiti Mwandamizi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), akitoa mada katika Kongamano la Wanawake jana.
Baadhi ya washiriki wa Kongamano la Wanawake lililodhaminiwa na CRDB kupitia Malkia Akaunti, wakimsikiliza Ofisa Masoko wa benki hiyo, Emmanuel Kiondo akitoa mada.
Baadhi ya washiriki wa Kongamano la Wanawake lililodhaminiwa na CRDB kupitia Malkia Akaunti, wakimsikiliza Ofisa Masoko wa benki hiyo, Emmanuel Kiondo akitoa mada.
Baadhi ya washiriki wa Kongamano la Wanawake lililodhaminiwa na CRDB kupitia Malkia Akaunti, wakimsikiliza Ofisa Masoko wa benki hiyo, Emmanuel Kiondo akitoa mada.
Msanii mwalikwa katika kundi la The Voice, akiimba kuwatumbuiza washiriki wa Kongamano la Wanawake wajasiriamali lililofanyika jana. Nyuma ni vijana wanaounda kundi la 'The Voice'.
Msanii mwalikwa katika kundi la 'The Voice', akiimba kwa hisia kutumbuiza washiriki wa Kongamano la Wanawake wajasiriamali lililofanyika jana. Nyuma ni vijana wanaounda kundi la The Voice.
'The Voice' wakikonga nyoyo za washiriki wa Kongamano la Wanawake lililofanyika jana jijini Dar es Salaam.
DAR ES SALAAM, Tanzania
KONGAMANO la Wajasiriamali Wanawake lilifanyika jana chini ya udhamini wa CRDB kupitia akaunti ya Malkia, ambapo benki hiyo ilitoa waelimishaji kadhaa waliotoa mada mbalimbali, zilizokuwa na nia ya kuwajengea wanawake uelewa wa namna sahihi za uwekezaji na faida zake
WAJASIRIAMALI Wanawake nchini, wametakiwa kutumia vema fursa zenye tija zipatikanazo katika Akaunti ya Malkia iliyo chini ya Benki ya CRDB, ili kuharakisha harakati za maendeleo yao kibiashara na kijamii.
Hayo yalisemwa na Ofisa Masoko Benki ya CRDB, Emmanuel Kiondo, alipokuwa akiwasilisha mada katika Kongamano la Wanawake, lililofanyika jijini Dar es salaam jana, likihusisha Wajasiriamali Wanawake.
Kiondo alisema kuwa, harakati za maendeleo kwa mwanamke ni muhimu kwa ustawi wa taifa na jamii na Malkia ya CRDB, ni njia sasahi itakayomuwezesha mjasiriamali huyo kuokoa pato lake ambalo awali lilikabiliwa na changamoto nyingi katika aina nyingine za uwekezaji.
“Malkia Akaunti ni mkombozi wa kweli wa mjasiriamali mwanamke, ikibeba tija nyingi na kumuepushia hadha zipatikanazo katika aina nyingine ya uwekezaji. Akaunti hii inatoa mkopo wa dharula wakati wa matatizo wa asilimia 80 ya akiba yako, bila kuathiri chochote,” alisema Kiondo.
Aliwakumbusha wanawake kuhakikisha wanauepuka kero na changamoto nzito zinazohatarisha harakati zao, kwa kuwekeza pesa zao kupitia akaunti hiyo, ambayo imewanufaisha wengi miongoni mwa wanawake wenye malengo tofauti.
Kongamano la Wanawake lilifanyika jana chini ya udhamini wa CRDB kupitia akaunti ya Malkia, ambapo benki hiyo ilitoa waelimishaji kadhaa waliotoa mada mbalimbali, zilizokuwa na nia ya kuwajengea wanawake uelewa wa namna sahihi za uwekezaji na faida zake.
Wakizungumzia kongamano hilo, baadhi ya washiriki walipongeza mada na ushuhuda uliotolewa na waelimishaji hao, ambao umewaongezea hamasa katika kukabiliana na changamoto mbalimbali za kibiashara na kutanua wigo wa maendeleo yao.
No comments:
Post a Comment