TANGAZO


Monday, May 13, 2013

Boko Haram lawateka watoto na wanawake


Kiongozi wa Boko Haram Abubakar Shekau
Wapiganaji wa kiisilamu wa Boko Haram wamewateka nyara wanawake na watoto katika kujibu hatua ya jeshi kuwakamata wake za wanachama wa kundi hilo pamoja na watoto wao.
Kiongozi wa Boko Haram, Abubakar Shekau, alitoa kanda ya video inayoonyesha wanawake na watoto waliowakamata.
Ikiwa hili litathibitishwa, watakuwa mateka wa kwanza raia wa Nigeria kutekwa nyara na kundi la Boko Haram.
Shekau pia alisema kuwa kundi hilo ndilo lilifanya mashambulizi mawili ya hivi karibuni Kaskazini Mashariki mwa nchi ambayo yaliwaacha takriban watu 240 wakiwa wameuawa.
Kundi hilo limekataa msamaha uliotolewa kwao na serikali ili waweze kuacha vurugu zao ambazo zimesababisha vifo vya watu 2000 katika miaka mitatu iliyopita.
Kundi la Boko Haram, limekuwa likituhumu vikosi vya usalama kwa kuwazuia kinyume na sheria jamaa za wapiganaji wa Boko Haram likisema kuwa kuachiliwa kwao itakuwa kikwazo cha kuwa na mwafaka wowote.
Kwenye kanda hiyo, Shekau hakusemna chochote kuhusu idadi ya wanawake na watoto waliokamatwa.
"tuliwakamata wanawake na watoto kadhaa pamoja na vijana barobaro,'' alisema bwana Shekau.

No comments:

Post a Comment