Pages

Sunday, April 21, 2013

Yanga yaukaribia Ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania

Mashabiki waYanga wakifuatilia mchezo kati ya timu hiyo na JKT Ruvu FC, uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo jioni. Yanga imeshinda mabao 3-0 na hivyo kuukaribia ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom nchini ikihitaji pointi moja tu kutawazwa kuwa bingwa wa ligi hiyo, ambao msimu uliopita ulinyakuliwa na mahasimu wao, Simba SC ya jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Kassim Mbarouk)

Damas Makwaya wa JKT Ruvu, akimtoka Nizar Khalfan wa Yanga wakati wa mchezo huo leo, Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Damas Makwaya wa JKT Ruvu, akijaribu kumzuia Simon Msuva wa Yanga katika mchezo huo.

Nashon Naftary (24) wa JKT Ruvu, akimtoka Khamis Kiiza wa Yanga.

Haruna Niyonzima wa Yanga, akimtoka Stanley Nkomola wa JKT Ruvu.

Nizar Khalfan wa Yanga, akijaribu kuwatoka Amos Mgisa (nyuma) na Madenge Ramadhan (28) wa JKT Ruvu. 

Simon Msuva wa Yanga akiwania mpira na Haruna Adolf wa JKT Ruvu.

David Luhende wa Yanga, akimtoka Hassan Kikutwa wa JKT Ruvu.

Hassan Kikutwa wa JKT Ruvu, akimkata kwanja David Luhende wa Yanga katika mchezo huo.

Madenge Ramadhan wa JKT Ruvu, akiupiga mpira kichwa huku ukisubiriwa na Nizar Khalfan wa Yanga.

Simon Msuva wa Yanga, akiwania mpira na Damas Makwaya wa JKT Ruvu katika mchezo huo.

Simon Msuva wa Yanga, akimtoka Damas Makwaya wa JKT Ruvu kwenda kufunga bao la kwanza la timu hiyo, iliyoibuka na ushindi wa mabao 3-0 katika mchezo huo.

Mashabiki wa Yanga wakifurahia bao la kwanza lililofungwa na Simon Msuva.

Nashon Naftary wa JKT Ruvu akimtoka Nizar Khalfan wa Yanga.

Wachezaji wa Yanga wakifurahia bao la pili la timu hiyo katika mchezo huo.

Wachezaji wa Yanga wapongezana baada ya kufanikiwa kupata bao la pili katika mchezo huo.

Mashabiki wa Yanga wakifurahia bao la pili la timu hiyo katika mchezo huo.

Mashabiki wa Yanga wakifurahia bao la tatu la timu hiyo katika mchezo huo, huku wakionesha mfano wa Kombe la Ubingwa wa Ligi ya Vodacom, katika kuonesha kwamba wako karibu na kunasa kombe hilo.

Mashabiki wa Yanga wakionesha furaha ya ushindi katika mchezo huo.

Ubao wa matangazo ukionesha Yanga mabao 3 na JKT Ruvu 0.

Haruna Niyonzima wa Yanga, akimiliki mpira huku akifuatwa na Ally Mkanga wa JKT Ruvu.

Haruna Niyonzima wa Yanga, akitafuta mbinu ya kumtoka Ally Mkanga wa JKT Ruvu.

Sosthenes Manyasi wa JKT Ruvu akimtoka Frank Domayo wa Yanga.

Sosthenes Manyasi wa JKT Ruvu, akimtoka Frank Domayo wa Yanga, huku Mbuyu Twite (kulia) wa timu hiyo, akimuangalia.

Shabiki wa Yanga akionesha vimbwanga vya kuukaribia ubingwa wa ligi hiyo kwa timu yake ya Yanga kwa kuonesha ishara ya kupiga picha za Tv kwa kamera bandia.

No comments:

Post a Comment