TANGAZO


Saturday, April 6, 2013

Sudan Kusini yaanza kuchimba mafuta tena



Sudan Kusini imeanza kuchimba mafuta tena na hivo kumaliza mzozo wa zaidi ya mwaka na Sudan uliogharimu nchi zote mbili mabilioni ya dola.
Mitambo ya mafuta ya Sudan
Sudan Kusini iliacha kutoa mafuta awali mwaka jana baada ya Sudan Kusini kumshutumu jirani yake kuwa inaitoza fedha nyingi kwa kuruhusu mafuta hayo kupita kwenye mabomba nchini humo hadi bandari ya Port Sudan.
Vita na tofauti nyengine bado hazikupatiwa suluhu, lakini waandishi wa habari wanasema kuanza kuchimba na kusafirisha mafuta ni ishara njema katika uhusiano baina ya nchi mbili hizo.
Asilimia-98 ya pato la Sudan Kusini linatokana na mafuta.

No comments:

Post a Comment