Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Biashara,Viwanda na Masoko, katika utekelezaji wa kazi za wizara hiyo, ukumbi wa mikutano wa Ikulu, mjini Zanzibar leo. Kushoto ni Makamo wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif Sharif Hamad.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Biashara,Viwanda na Masoko, katika utekelezaji wa kazi za wizara hiyo, ukumbi wa mikutano wa Ikulu, mjini Zanzibar leo. Kushoto ni Makamo wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif Sharif Hamad.
Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar.
08.4.2013
WIZARA ya Afya imeeleza kuwa inaendelea na
mchakato wa kutafuta vifaa ili kuweza kuanzisha redio maalum (Afya FM Redio), itakayosadia katika utoaji elimu ya afya kwa jamii.
Hayo yameelezwa leo na uongozi wa Wizara ya Afya
katika mkutano kati ya uongozi huo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, katika kuangalia utekelezaji wa
mpango kazi wa Wizara hiyo kwa kipindi cha Julai, 2012- Machi, 2013.
Katika mkutano huo, uliofanyika Ikulu mjini Zanzibar, ulihudhuriwa na Makamu wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif Sharif Hamad, Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Idd na Katibu wa Baraza la Mapinduzi, ambaye pia ni Katibu Mkuu Kiongozi, Dk.
Abdulhamid Yahya Mzee, ambapo Wizara hiyo ilieleza ilivyoweka
azma hiyo kwa lengo la kuwasaidia wananchi kupata taarifa mbali
mbali za afya.
Uongozi huo chini ya Waziri wake Mhe. Juma Duni, alieleza
kuwa kuwepo kwa redio hiyo kutasaidia kwa kiasi kikubwa kutengeza na kuonesha
vipindi kadhaa vya redio ambayo vitaelimisha jamii juu ya masuala mbali mbali ya
afya.
Wizara hiyo ilieleza kuwa bado inaendelea kutoa elimu ya
afya kwa wananchi ili kuweza kujikinga na maradhi mbali mbali
yakiwemo ya kuambukiza na yasio ya kuambukiza ambapo jumla ya vipindi 69 vya
elimu ya afya vimesharushwa hewani kupitia redio na televisheni hapa
nchini.
Mhe. Juma Duni alieleza kuwa sekta ya afya ni miongoni
mwa sekta muhimu katika maendeleo ya taifa lolote ulimwenguni hivyo ipo haja ya
kuhakikisha Wazanzibari wote wanapata huduma bora za afya.
Alisisitiza kuwa Wizara ya Afya ndiyo iliyopewa jukumu la
kuhakikisha huduma za afya za kinga na tiba zinaimarika na kuendeleza ustawi wa
watu wa Zanzibar kwa kutilia mkazo zaidi wanawake, watoto na makundi wengine
yanayoishi katika mazingira magumu.
Aidha, uongozi huo ulieleza kuwa tayari hatua za awali za
ujenzi wa wodi ya mama wajawazito katika hospitali ya Wete zimeshaanza ikiwa ni
pamoja na kuitisha tenda ya kutafuta wakandarasi watakaosimamia ujenzi wa wodi
hiyo.
Wizara hiyo ilieleza kuwa ujenzi huo unasimamiwa na Mradi
wa kusaidia kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi chini ya ufadhili
wa Benki ya Maendeleo ya Afrika ADB na unatarajiwa kumaliza ifikapo Juni,
2014.
Pamoja na hayo, Wizara hiyo ilieleza azma
yake ya kujenga jengo la ghorofa moja la Ofisi ya Mradi Shirikishi wa Afya ya
Uzazi na Mtoto, jengo ambalo linajengwa katika eneo la hospitali ya Wagonjwa wa
Akili Kidongo Chekundu.
Ilielezwa kuwa ujenzi uko katika hatua nzuri na tayari
ghorofa ya juu imeshajengwa na kilichobaki ni kuendelea na hatua za mwisho za
ujenzi ikiwemo kuezekwa na kumalizwa matengenezo ya mwisho.
Kwa upande wake Dk. Shein alisisitiza haja
ya kutoa elimu ya afya kwa wananchi hasa juu ya maradhi ya Malaria kwani
Zanzibar inatambulika duniani kote kutokana na mafanikio iliyoyapata hivyo kuna
haja ya kusonga mbele badala ya kurudi nyuma.
Alieleza kuwa ipo haja ya kuongeza nguvu na kasi ya
kuelimishana juu ya maradhi hayo huku akieleza juhudi za serikali katika
kuondosha maradhi hayo ambazo zinapaswa kuungwa mkono na wananchi wote.
Sambamba na hayo, Dk. Shein alitoa pongezi kwa Wizara
hiyo kwa juhudi zake inazoendelea kuzichukua katika kutoa huduma ya afya kwa
wananchi huku akiwasisitiza watendaji wa wizara hiyo kuendelea kutoa huduma bora
kwa wananchi.

No comments:
Post a Comment