TANGAZO


Tuesday, April 16, 2013

Makamu wa Rais Dk. Bilal afungua mkutano wa siku mbili wa udhibiti wa huduma za kiuchumi barani Afrika jijini Arusha

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati akifungua rasmi Mkutano wa Kimataiafa wa siku mbili wa Udhibiti wa Huduma za Kiuchumi barani Afrika, ulioshirikisha Mataifa mbalimbali kutoka Bara la Afrika, ulioanza leo, Aprili 16, 2013 kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC jijini Arusha. (Picha zote na OMR)

Baadhi ya washiriki wa mkutano huo, wakiwa ukumbini wakiangalia makabrasha yao yenye maelezo mbalimbali kuhusu mkutano huo, wakati wakimsikiliza Makamu wa Rais Dk. Bilal wakati akiwahutubia.

Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akizindua Kitabu cha Udhibiti wa Huduma za Kiuchumi barani Afrika, wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa wa siku mbili wa Udhibiti wa Huduma za Kiuchumi barani Afrika, ulioshirikisha Mataifa mbalimbali ya hilo, ulioanza leo Aprili 16, 2013, ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC, jijini Arusha. Kitabu hicho kimetungwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Kazi Maalum), Profesa, Mark Mwandosya. Kulia ni Waziri wa Maji, Profesa. Jumanne Maghembe na kushoto ni Mkurugenzi wa Ewura, Haruna Masebu.

Baadhi ya washiriki wa mkutano huo, wakiwa ukumbini humo, wakimsikiliza Makamu wa Rais Dk. Gharib Bilal wakati alipokuwa akiwahutubia.

Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akionesha kitabu cha udhibiti wa huduma za kiuchumi barani Afrika, baada ya kukizindua rasmi, wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Kimataifa wa siku mbili wa udhibiti wa huduma za kiuchumi katika bara hilo, ulioshirikisha mataifa mbalimbali ya Bara la Afrika, ulioanza leo Aprili 16, 2013, ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC jijini Arusha. Kitabu hicho kimetungwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Kazi Maalum) Profesa Mark Mwandosya (kulia). Katikati ni Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe.

Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akionesha zawadi baada ya kufungua mkutano wa Kimataifa wa siku mbili wa Udhibiti wa Huduma za Kiuchumi Bara la Afrika, kutoka kwa Mkurugenzi wa Ewura, Haruna Masebu. Mkutano huo ulioshirikisha mataifa mbalimbali ya Bara la Afrika, umeanza leo Aprili 16, 2013 katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC jijini Arusha.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mkutano huo baada ya ufunguzi.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mkutano huo baada ya ufunguzi.

No comments:

Post a Comment