 |
Maofisa wa Kikosi cha cha uokoaji cha Zimamoto, wakiwa katika hafla ya Rais Jakaya Kikwete, ukumbi wa Karume, Viwanja vya Sabasaba Dar es Salaam leo, kutoa shukurani na kuwatunuku vyeti, washiriki walioshiriki katika uokoaji wa wananchi waliopata ajali ya kudondokewa na jengo la ghorofa 16 jijini hivi karibuni. (Picha zote na Kassim Mbarouk)
 |
Baadhi ya wapiganaji wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania wakiwa katika hafla hiyo, kabla ya Rais Jakaya Kikwete kuwasili kwenye ukumbi wa Karume, Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
|
Baadhi ya Maofisa wa Jeshi la Polisi, wakiwa katika hafla hiyo, kabla ya Rais Kikwete kuwasili kwenye ukumbi wa Karume, Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
|
 |
| Maofisa wa Msalaba Mwekundu, wakiwa katika hafla ya Rais Jakaya Kikwete, ukumbi wa Karume, Viwanja vya Sabasaba Dar es Salaam leo, kutoa shukurani na kuwatunuku vyeti, washiriki walioshiriki katika uokoaji wa wananchi waliopata ajali ya kudondokewa na jengo la ghorofa 16 jijini hivi karibuni. |
 |
| Viongozi wa Dini, Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum (wa pili kulia) na Mchungaji George Fupe (wa pili kushoto) na Shikh Ismaili wakiwa katika hafla hiyo. |
 |
| Rais Jakaya Kikwete akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki (wa pili kushoto), wakati wa hafla hiyo. |
 |
| Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum, akitoa dua katika hafla hiyo. |
 |
| Mchungaji George Fupe, akitoa dua katika hafla hiyo. |
 |
| Sheikh Ismail wa Jumuiya ya Khoja Ithna Asheri, akitoa dua katika hafla hiyo. |
 |
| Rais Jakaya Kikwete akitoa cheti cha Shukurani kwa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, ambayo ilipokelewa na Katibu Tawala wa Mkoa huo, Theresia Mmbando. |
 |
| Rais Jakaya Kikwete akitoa cheti cha Shukurani kwa mwakilishi wa Kampuni ya Ujenzi ya China ya CC. |
 |
| Rais Jakaya Kikwete akitoa cheti cha Shukurani kwa mwakilishi wa Jeshi la Polisi Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Afande Suleiman Kova. |
 |
| Rais Jakaya Kikwete akitoa cheti cha Shukurani kwa mwakilishi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), katika hafla hiyo. |
 |
| Rais Kikwete akitoa cheti cha Shukurani kwa Waziri wa TAMISEMI, Hawa Ghasia. |
 |
| Rais Jakaya Kikwete, akimkabidhi cheti cha kutambua mchango wa huduma za uokoaji, Mwakilishi wa Kampuni za Africa Media Group, Mhariri wa habari wa kituo cha televisheni cha Channel Ten, Esther Zelamula. |
 |
| Rais Kikwete akitoa cheti cha Shukurani kwa kijana wa Nigeria anayeishi Zanzibar, Yussuf Abubakar katika kutambua mchango wake kwenye uokoaji huo. |
 |
| Baadhi ya wapiganaji wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania wakiwa katika hafla hiyo, wakimsikiliza Rais Kikwete alipokuwa akiwahutubia katika kutoa shukurani zake kwa watu walioshiriki katika uokoaji huo. |
 |
| Baadhi ya Maofisa wa ngazi ya juu wa Jeshi la Polisi na Usalama, wakiwa katika hafla hiyo, wakimsikiliza Rais Kikwete alipokuwa akiwahutubia katika kutoa shukurani zake kwa watu walioshiriki katika uokoaji huo. Kushoto ni Kamanda Suleiman Kova. |
 |
| Rais Jakaya Kikwete akihutubia leo, wakati alipokuwa akitoa shukurani zake kwa watu walioshiriki katika uokoaji wa wananchi waliodondokewa na jengo la ghorofa 16 jijini Dar es Salaam hivi karibuni. |
 |
| Baadhi ya wananchi na wageni mbalimbali waalikwa waliohudhuria katika hafla hiyo, wakimsikiliza Rais Jakaya Kikwete, wakati alipokuwa akiwahutubia ukumbini hapo. |
 |
| Rais Jakaya Kikwete Jakaya Kikwete akiwaeleza jambo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mecki Sadiki na Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema wakati alipokuwa akizungumza na mlemavu aliyeacha kuuza na kutumia madawa ya kulevya, Shaaban Selemani wakati alipokuwa akikumbushia ahadi ya Bajaj aliyoahidiwa na Rais Kikwete, baada ya kumalizika hafla hiyo. |
Rais Jakaya Kikwete akiwaaga, waokoaji wa Kikosi cha Zima Moto pamoja na wapiganaji wa Jeshi la Wananchi na wageni mbalimbali waliokuwa katika hafla hiyo.
No comments:
Post a Comment