Pages

Thursday, April 18, 2013

Hukumu ya Kesi ya Ponda na wenzake yaahirishwa hadi Mei 9, ulinzi waimarishwa, Waislamu wapagawa

Katibu wa Taasisi na Jumuiya za Kiislamu, Sheikh Issa Ponda, akitoka kwenye chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu mara baada ya kesi inayomkabili pamoja na wenzake 49, kuahirishwa kutolewa hukumu baada ya hakimu anayeisikiliza, Victoria Nongwa kuwa safarini nje ya Dar es Salaam. Pamoja na kutokutolewa hukumu ya kesi hiyo, Jeshi la Polisi, Magereza pamoja na Usalama, walikuwa wamejitayarisha kukabiliana na ghasia zozote ambazo zingelitokea kutoa kwa wafusi wa Sheikh Ponda na jamaa zake, ambao walikuwa wamekusanyika na wengine kulala mahakamani hapo kusubiri hukumu ya kesi hiyo. (Picha zote na Kassim Mbarouk)

Katibu wa Taasisi na Jumuiya za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda na msaidizi wake, Saleh Mukadam, wakiongozwa na askari Magereza kuelekea kwenye gari la mahabusu kurejeshwa Mahabusu ya Segerea kusubiri kuendelea na kesi yao, ambayo itatajwa tena Mei 2 na kisha hukumu yake kutolewa Mei 9 mwaka huu, mahakamani hapo.

Katibu wa Taasisi na Jumuiya za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda na msaidizi wake, Saleh Mukadam, wakiongozwa na askari Magereza kuelekea kwenye gari kwa ajili ya kurejeshwa Mahabusu ya Segerea kusubiri kuendelea na kesi yao, ambayo itatajwa tena Mei 2 na kisha hukumu yake kutolewa Mei 9, mwaka huu, mahakamani hapo.

Katibu wa Taasisi na Jumuiya za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda na msaidizi wake, Saleh Mukadam, wakijitayarisha kupanda kwenye gari kwa ajili ya kurejeshwa Mahabusu ya Segerea kusubiri kuendelea na kesi yao, ambayo itatajwa tena Mei 2 na kisha hukumu yake kutolewa Mei 9, mwaka huu, mahakamani hapo.

Mshitakiwa Saleh Mukadam, anayeshitakiwa pamoja na Sheikh Ponda akipanda kwenye gari hilo kwa ajili ya kurejeshwa Mahabusu ya Segerea kusubiri kuendelea na kesi yao, ambayo itatajwa tena Mei 2 na kisha hukumu yake kutolewa Mei 9, mwaka huu, mahakamani hapo.

Askari Polisi wa Kikosi cha Mbwa na Farasi wakiwa tayari kwa ajili ya kupambana na jambo lolote ambalo lingelitokea mahakamani hapo leo. 

Askari Polisi wa Kikosi cha Farasi wakiwa wamefunga barabara ya UWT, huku wakiwa wamejiweka tayari kupambana na jambo lolote ambalo lingelitokea mahakamani hapo leo. 

Askari Polisi wa Kikosi cha Mbwa na askari kanzu, wakiwa wamejiweka tayari kupambana na jambo lolote ambalo lingelitokea mahakamani hapo leo. 

Baadhi ya kundi la Waislamu waliokuwepo mahakamani hapo kusubiri kutolewa huku ya kesi hiyo, wakiwa nje ya Mahakama hiyo, kusubiri kinachoendelea.

Gari la Kikosi cha askari wa Kutuliza Ghasia (FFU), wakiongoza msafara wa washitakiwa Sheikh Issa Ponda na Saleh Mukadam, kurejeshwa mahabusu ya Segerea baada ya kuaghirishwa kutolewa kwa hukumu ya kesi yao hiyo leo.

Baadhi ya kundi la Waislamu waliokuwepo mahakamani hapo kusubiri kutolewa huku ya kesi hiyo, wakishangilia baada ya kuona magari yaliyowabeba washitakiwa hao, yakiondoak kwa mwendo wa kasi kuelekea Mahabusu ya Segerea jijini Dar es Salaam leo.

Kundi la Waislamu waliokuwepo mahakamani hapo kusubiri kutolewa huku ya kesi hiyo, wakishangilia gari lililowabeba washitakiwa hao, wakati likipita mbele yao kwa mwendo wa kasi kuelekea Mahabusu ya Segerea jijini Dar es Salaam leo.

Kundi la Waislamu waliokuwepo mahakamani hapo kusubiri kutolewa huku ya kesi hiyo, wakishangilia kwa kusema Takbir, gari lililowabeba askari Magereza waliokuwa wakiwasindikiza washitakiwa hao, wakati likipita mbele yao kwa mwendo wa kasi kuelekea Mahabusu ya Segerea jijini Dar es Salaam leo.


Kundi la Waislamu waliokuwepo mahakamani hapo kusubiri kutolewa huku ya kesi hiyo, wakishangilia kwa kusema Takbir, gari lililowabeba askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), waliokuwa wakiwasindikiza washitakiwa hao, wakati likipita mbele yao kwa mwendo wa kasi kuelekea Mahabusu ya Segerea jijini Dar es Salaam leo.

Kundi la Waislamu waliokuwepo mahakamani hapo kusubiri kutolewa huku ya kesi hiyo, wakishangilia kwa kusema Takbir, gari la maji ya kuwasha, lililokuwa likiwasindikiza washitakiwa hao, wakati likipita mbele yao kwa mwendo wa kasi kuelekea Mahabusu ya Segerea jijini Dar es Salaam leo.

Baadhi ya kundi la Waislamu waliokuwepo mahakamani hapo kusubiri kutolewa huku ya kesi hiyo, wakiwa nje ya Mahakama hiyo, wakishangaa baada ya washitakiwa hao kuondoka mahakamani hapo leo.

No comments:

Post a Comment